Header Ads Widget

RIDHIWANI ATAKA VIJANA WANAOJIAJIRI KUPITIA MITANDAO WAJISAJILI BRELA.


 

NAIBU Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete amewataka vijana wanaofanya shughuli zao kwenye mitandao kujisajili kisheria.


Akizungumza na baadhi ya vijana wanaofanya shughuli zao kwenye mitandao na  kujisajili na BRELA kwenye maonyesho ya biashara na uwekezaji ya Mkoa wa Pwani alisema ni vema wakawa kisheria.


Ridhiwani alisema kuwa vijana wengi wamejiajiri kupitia mitandao na kuonyesha uwezo wao imefika wakati wasajili ili waendane na sheria inavyotaka.


"Nawapongeza vijana kwa kuchangamkia fursa za kujiajiri kwenye mitandao ambapo wanajiongezea kipato hili ni soko kubwa kwa vijana,"alisema Ridhiwani.


Aidha alisema kuwa serikali inatengeneza mazingira mazuri ya vijana kufanya shughuli za kujiongezea kipato.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI