Mgeni rasmi wa mahafali ya 11 ya shule ya sekondari ya Agustivo iliyopo Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma, James Mungo akizungumza katika mahafali hayo.Mhitimu akipokea cheti katika mahafali ya 11 ya shule ya sekondari Agustivo Sehemu ya wahitimu wa shule ya sekondari Agustivo Mkuu wa shule ya sekondari ya Agustivo, Mosses Mapunda. Mmiliki wa shule ya sekondari Agustivo, Joseph Mdaka
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Na Amon Mtega, Mbinga.
MENEJA wa Usalama na Afya wa kampuni ya uchimbaji wa makaa ya mawe ya Ruvuma Coal Limited yaliopo kata ya Ruanda Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma James Mungo amewataka wanafunzi waliohitimu kidato cha nne wa shule ya Sekondari ya Agustivo iliopo mjini Mbinga kuendelea kufanya vizuri mitihani yao ya mwisho ili waweze kusonga mbele kwa Elimu ya ngazi zinazofuatia.
Mungo ametoa wito huo wakati akiwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya 11 ya shule hiyo ambayo yenye kidato cha kwanza hadi cha sita (HIGH SCHOOL)huku wahitimu wa kidato cha nne ni 51 kati ya 55 ambapo wanafunzi wanne wamekutwa na sababu mbalimbali zikiwemo za mdondoko.
Meneja huyo huyo amesema kuwa Shule hiyo ina historia ya kufanya vizuri kwenye mitihani yao hivyo kusiwepo baadhi yao kuishi na historia hiyo bali waendelee kuitunza historia hiyo kwa kufanya vizuri mitihani yao ya mwisho.
Amesema kuwa kumekuwepo kwa baadhi ya wanafunzi wakihitimu darasa la saba au kidato cha nne wanajiona tayari wameshafikia malengo ya Elimu kumbe bado safari inaendelea ,hivyo ni vema wahitimu wajipange kuendelea na masomo ya hatua nyingine kwa kuongeza ufaulu.
Hata hivyo mgeni rasmi huyo ambaye ametoa mipira ya miguu na mipira ya pete kwenye shule amesema kuwa kampuni yao ina kawaida ya kupita kuangalia baadhi ya changamoto kwenye shule mbalimbali za Wilayani humo hivyo kwa sasa baadhi ya shule zina upungufu wa vitabu vya masomo mbalimbali ambavyo kampuni itasaidia ikiwemo na shule ya Sekondari Agustivo.
Awali mwanafunzi Joseph Madilu akisoma risala ya wahitimu hao amesema kuwa Shule hiyo yenye mazingira mazuri ya kusomea ambayo ni rafiki wa mwanafunzi inakabiliwa na changamoto ya upungufu wa baadhi ya vitabu ili viweze kukidhi kwa wanafunzi waliopo shuleni hapo.
Madilu akisoma risala hiyo amesema kuwa licha ya kuwepo kwa changamoto ya upungufu wa baadhi ya vitabu lakini wanafunzi wake wamekuwa wakifaulu kwa asilimia karibu 100 kutokana na jitihada na usimamizi wa uongozi uliopo shuleni hapo.
Kwa upande wake mmiliki wa Shule hiyo Joseph Mdaka akitoa neno la shukrani amewapongeza Wazazi na Walezi wa wanafunzi hao kwa kusimama na shule hiyo bega kwa bega kuhakikisha wanafunzi hao wanahitimu vema.
Mdaka ambaye pia ni mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mbinga Mkoani humo amesema kuwa Wazazi na Walezi wakisimama imara katika suala nzima la kuwasaidia watoto kupatiwa Elimu hakuna mtoto ambaye ambaye atakaye acha shule.
Naye mkuu wa shule hiyo Mosses Mapunda amesema kuwa wanafunzi hao wameandaliwa ipasavyo na wameiva kitaaluma hivyo wanaimani watafanya vizuri kwenye mitihani yao ya mwisho inayoenda kuanza hivi karibuni.
0 Comments