Baada ya Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi lilibaini kuwa mtuhumiwa huyo siyo mtumishi wa Idara ya Usalama Wa Taifa na gari alilokamatwa nalo aina ya VW TOURAGE lenye namba za usajili T 858 DVE rangi nyeusi amemtapeli Ndugu Mohamed Nassoro mfanyabiashara wa magari Magomeni Jijini Dar Es Salaam baada ya kujitambulisha kuwa ni mtumishi kutoka Idara ya Usalama wa Taifa kwa makubaliano ya malipo ya jumla ya Shilingi Milioni 18,500,000/=. Hata hivyo, mtuhumiwa hakulipa kiasi chochote cha fedha na kutoweka na gari hilo. Mtuhumiwa amefikishwa Mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.
Katika tukio lingine, Jeshi la Polisi Mkoani Iringa Oktoba 03,2022 majira ya saa Tatu asubuhi katika kijiji cha igingilanyi Kata ya Isimani Wilaya na Mkoa wa Iringa, lilifanikiwa kukamatwa Mtambo(WHEEL LOADER CARTPILLE) wenye namba T 322 CAF mali ya kampuni ya DB SHAPRIYA & CO, LTD yenye thamani ya Shilingi Milioni 250,000,000/= na mtuhumiwa mmoja amekamatwa ambaye ni mwanaume, miaka 42, ambaye ni fundi na Mkazi wa Nduli akiwa na mali za wizi zilizofunguliwa kutoka kutoka kwenye Mtambo huo, ambazo ni Engine Model no 3126, Rejeta 1, Madguard 4, Hydrolic Pipe, Wiring System pamoja na Fan Guard na Propeller shaft.
Katika tukio lingine, Jeshi la Polisi mkoani Iringa limefanikiwa kumkamata Pius Miki mkazi wa Wilolesi kwa tuhuma za kuvunja na kuiba katika nyumba ya ndugu yake Felix Miki ambapo baada ya mahojiano mtuhumiwa amekiri kutenda kosa hilo na kuonyesha mali alizoiba katika nyumba hiyo ambazo ni Runinga aina ya TELEFUNKEN inch 55, Jiko la Umeme, Jokofu, Godoro, Sofa, pamoja na Mitungi ya Gas 43 kampuni tofauti Mikubwa 5, na Midogo 38. Watuhumiwa watafikishwa Mahakamani upelelezi utakapokamilika.
0 Comments