Header Ads Widget

JENERALI MUHOOZI KAINERUGABA AMESEMA ANAFIKIRIA KUMKAMATA WAKILI ALIYEMFUNGULIA KESI.


Mkuu wa zamani wa Jeshi la Ardhini Uganda, Muhoozi Kainerugaba ambaye ni Mtoto wa Rais Museveni amesema amezipata taarifa za Wakili Apollo Mboya kutoka nchini Kenya kumfungulia kesi ya uhaini katika Mahakama ya Sheria ya Nairobi kwa kutishia usalama wa Kenya ambapo Muhoozi hajashtushwa zaidi ya kusema anafikiri labda amkamate Wakili Mboya.


Kwenye kesi aliyofungua Wakili Mboya amedai Muhoozi amefanya uhaini kwa kutumia ukurasa wake wa Twitter na kwamba ametishia usalama wa Kenya kwa kusema yeye na Jeshi lake wataliteka Jiji la Nairobi ndani ya Wiki moja tu huku akisema licha ya kosa hilo Rais wa Uganda ambaye ni Baba yake Muhoozi aliamua kumzawadia kwa kumpandisha cheo na kuwa Jenerali.


Kwenye kesi yake hiyo Wakili Mboya amewajumuisha pia kwenye mashtaka yake Mkuu wa Polisi Kenya (IGP) na DPP wa Kenya kwa kushindwa kumchukulia hatua Muhoozi licha ya kutishia usalama wa Kenya.


Mboya ametaka Mahakama ichukulie suala hilo kuwa ni la dharura na iagize kuwa Muhoozi ana kesi ya kujibu pia ametaka Mahakama iwaagize IGP na DCI kupeleka Mahakamani nyaraka zinazoonesha kuwa wamefanya uchunguzi na wamechukua hatua dhidi ya tishio la usalama wa Kenya lililotolewa na Muhoozi.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS