Header Ads Widget

WAKILI AMFUNGULIA KESI YA UHAINI MTOTO WA RAIS MUSEVENI

Wakili Apollo Mboya kutoka nchini Kenya amefungua kesi katika Mahakama ya Sheria ya Nairobi akitaka Mkuu wa zamani wa Jeshi la Ardhini la Uganda Muhoozi Kainerugaba ambaye ni Mtoto wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni ahukumiwe kwa kosa la uhaini kwa kutishia usalama wa Kenya.


Wakili Mboya amedai Muhoozi amefanya uhaini kwa kutumia ukurasa wake wa Twitter na kwamba ametishia usalama wa Kenya kwa kusema yeye na Jeshi lake wataliteka Jiji la Nairobi ndani ya Wiki moja tu huku akisema licha ya kosa hilo Rais wa Uganda ambaye ni Baba yake Muhoozi aliamua kumzawadia kwa kumpandisha cheo na kuwa Jenerali.


Kwenye kesi yake hiyo Wakili Mboya amewajumuisha pia kwenye mashtaka yake Mkuu wa Polisi Kenya (IGP) na DPP wa Kenya kwa kushindwa kumchukulia hatua Muhoozi licha ya kutishia usalama wa Kenya.


Mboya ametaka Mahakama ichukulie suala hilo kuwa ni la dharura na iagize kuwa Muhoozi ana kesi ya kujibu pia ametaka Mahakama iwaagize IGP na DCI kupeleka Mahakamani nyaraka zinazoonesha kuwa wamefanya uchunguzi na wamechukua hatua dhidi ya tishio la usalama wa Kenya lililotolewa na Muhoozi.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS