Header Ads Widget

HALMASHAURI YA TANGA YAPATA MILIONI 585 ZA UJENZI WA MADARASA 29.

 


Na Amina Said, Tanga


Halmashauri ya jiji la Tanga imepata kiasi cha sh.Milioni  585 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 29 ya shule saba katika Halmashauri hiyo


Akizungumza katika baraza la Madiwani la Halmashauri  ya jiji la Tanga yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano ya jiji Mkurugenzi wa Halmashauri Dr.Sipora Liana alisema watahakikisha wanatekeleza agizo la Rais Samia Suluhu Hassan kuhakikisha ifikapo disemba kazi ya ujenzi inakamilika



Aidha alisema kwamba tayari pesa imeshaingizwa tangu tarehe 25 mwezi huu katika mafungu,hivyo kama Halmashauri kwa ajili ya utekelezaji wa miradi na wao kama wataalmu nao wamejigawa katika mafungu kuhakikisha kazi inaendelea


"Sisi wataalamu na waheshimiwa tayari misingu ilishachimbwa wapo katika utaratibu wa kutafuta mafundi na matofali yameshasambazwa katika shule zote hivyo wanaendelea kupeleka mchanga na simenti kwa ajili ya kuhakikisha ujenzi unakamilika


"Shule zenyewe ni shule ya msingi Kiyomoni iko kata ya Maweni shule ya Sekondari Ummy Mwalim kata ya Maweni Tanga Tec,shule ya Hoten Sekondari shule ya Marungu shule ya Kirare na Chongoleani "alisema Dr.Sipora 


Aidha waliomba Tamisemi kuingiza pesa katika mafungu ili kusimamia ujenzi huo ili ufanyike usiku na mchana kwani wameweka taa kubwa zitakazowawezesha kufanya kazi hadi usiku


Kwa upande wake Diwani wa kata ya Ngamiani Kaskazini Fahad Abdalah alipongeza Rais Samia Suluhu  Hassan kwa kuwajali wananchi wa jiji la Tanga kwa kuhakikisha wanapata fedha kawa ajili ya ujenzi wa madarasa




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI