Header Ads Widget

HALMASHAURI YA BARIADI YAPOKEA TSH BILIONI 75 KWA AJILI YA UJENZI WA KITUO CHA KUPOOZA UMEME

 


Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu imepokea kiasi cha Sh75 Bilioni kwa ajili ya ujenzi wa wa Kituo Cha Kupozea Umeme unaotoka Gridi ya Taifa ya Shirika la umeme nchini (Tanesco) kuingia ndani ya Mkoa wa Simiyu.

Kauli hiyo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Bw. Lupakisyo Kapange katika Maombezi Maalumu yaliyowakutanisha Waumini wa Dini zote za Kikiristo na wa Dini za Kiislamu Mkoani Simiyu, ambopo Mkuu wa Wilaya hiyo ya Bariadi Bw. Lupakisyo Kapange aliyasema hayo katika ibada Maalum iliyoandaliwa na Waumini wote wa Madhehebu hayo kumuombea Rais wa Nchi Samia Suluhu Hassan pamoja na kuimbea Nchi ya Tanzania kuendelea kuwa na amani na utulivu.

Katika Maombezi hayo yaliyofanyika Viwanja vya Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu ambapo aliwataka Wakazi wa Wilaya hiyo na Mkoa wa Simiyu kwa ujumla kuendelea kumuombea Rais Samia aendelee kutekeleza majukumu yake kwa weledi.


Alisema kuwa Tangu kuingia kwa Rais Samia madarakani, Wilaya yake imeweza kutekeleza Miradi mbali mbali ya kimkakati ambapo Tangu kwa kuanzishwa kwa Wilaya hiyo haijawahi kupata fedha kuanzisha Shule shikizi.

Alisema kuwa kupitia uongozi wa Rais Samia, Wilaya yake imefanya ujenzi wa Vyumba vya Madarasa 117 kwa Sh800 Milioni ambapo pia kiasi Cha Sh285 zilitolewa na Rais kwa ajili ya Ujenzi wa Vyumba hivyo vya Madarasa kwa Bariadi Vijijini.

“Pia tumefanya ujenzi wa Vituo Vitatu vipya vya Afya  kwa Sh900 Milioni pamoja na kufanya maboresho kwa Hospitali ya Somanda iliyoko Wilayani Bariadi kwa kujenga WiFi ya Kinamama na Watoto kwa gharama za Sh800 katika eneo la Dutwa,” alisema.

Bw. Kapange aliongeza kuwa mbali na ujenzi wa miundombinu ya hospitali pia kwa Mwaka huu wa fedha Wilaya ya Bariadi imeanza ujenzi na kufanyia ukarabati wa Barabara za Vijijini ambapo kiasi cha Sh5.8 Bilioni zimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa Barabara mpya zitakazo unganisha maeneo mbali mbali ya Wilaya hiyo na Mkoa kwa ujumla.

Alisema kuwa pia Wilaya hiyo imetengewa fedha kiasi Cha Sh5 Bilioni kwa ajili ya ujenzi wa Chuo Cha Ufundi Stadi (Veta) ambacho kutakuwa ni chio cha kwanza Cha Ufundi kwa Mkoa wa Simiyu.

“Wito wangu Ni Wakazi wa Bariadi tuendelee kumuombea Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan aendelee kutekeleza majukumu yake na kufungua fursa nyingi za kimaendeleo kwa Wilaya yetu na Mkoa wa Simiyu kwa ujumla,” alisema.

Akitoa salamu za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Simiyu, Mwenyekiti wa Chama hicho Wilaya ya Bariadi Bi. Juliana Mahongo alisema kuwa alisema kuwa maombezi hayo Ni Maalumu kwa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Taifa kwa ujumla sababu yatasaidia katika kuimalisha amani na utulivu ndani ya nchi na kutatua changamoto kadhaa ambazo zinaendelea kulikumba Taifa.

“Tunapoenda kufanya maombezi haya kwa Rais Samia pia tufanye maombezi kwa ajili ya upatikanaji wa mvua ya kutosha kwa ajili ya kuimalisha upatikanaji wa chakula Nchini ili Rais wetu asiwe na wasiwasi juu ya Afya na Hali ya kinaisha ya Watanzania,” alisema.

Katibu wa CCM Mkoa wa Simiyu, Bw. Masanja Salu alisema kuwa kufanyika kwa maombezi haya ambayo yamekutanisha Dini zote kuliombea Taifa ni Jambo la kihistoria kwa Nchi.

Naye Padre Peter Mkunya wa Kanisa Katoriki Wilaya ya Bariadi, Bw. Peter Mkunya alisema kuwa kazi anahofanya Rais wetu ni kubwa kwa kuwa anayafanya yote haya Kama mama mzazi anapokuwa anamlea mtoto wake mchanga.

“Mama mzazi anapomlea Mtoto wake mchanga atafanya yote awezayo kwa ajili Afya na uhai wa mtoto wake ndio anahofanya Rais wetu kwa Sasa,” alisema.

Sheikh Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Bw. Jumaa Athumani Alisema kuwa kusanyiko hili lilikutanisha Dini zote limeandaliwa na ofisi ya Mkuu wa Wilaya pamoja na Viongozi wa Dini zote Mkoa wa Simiyu ambalo linalenga kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan atekeleze majukumu yake na kutatua changamoto kadhaa zinazowakumba Wananchi wake.

Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI