Header Ads Widget

KIKWETE : BRELA ENDELEENI KUTOA HUDUMA ZA USAJILI KWENYE MIKUSANYIKO MBALIMBALI

 


Na Scolastica Msewa, Kibaha

Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba  na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete amewapongeza  Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA)  kwa huduma wanayoendelea kuitoa ya usajili kwenye Maonesho ya tatu ya  Uwekezaji na  Bashara yanayoendela  kweye viwanja vya Stendi ya Zamani Mailimoja Kibaha Mkoani Pwani.


Amesema hayo wakati alipofika kutembelea kwenye banda la BRELA katika mkoa Pwani katika Maonyesho ya tatu ya Uwekezaji na Biashara yanayoendelea katika viwanja vya standi ya mailmoja na kufanikiwa kumkabidhi  kijana  Idriss Njeru cheti chake cha usajili baada ya kukamilisha hatua za usajili.


"Lazima vijana  mjifunze kufanya kazi kwa kufuata kanuni na taratibu za serikali kama jinsi wewe ulivyojisajili nakupongeza sana" amesema  Mheshimiwa Kikwete.


Ameongeza kwa kusema kuwa vijana lazima mjisajili hasa kwa Kampuni  za Teknolojia kwani ukijisajili unakuwa  vizuri na unakuwa na ulinzi katika utendaji wa kazi zako".


Endeleeni  kufanya kazi kwa njia  halali na kuingia katika mfumo rasmi  wa serikali, hongera sana kwa kupata usajili kwani  hii ni sehemu ya kuchangia pato la taifa "amesema Kikwete.


Nenda ukawe balozi  mzuri  kwa vijana wenzako kua mjanja  ni pamoja na kujisajili BRELA huku ukifanya kazi nzuri zenye kuzingatia maadili ya Mtanzania  kwani kuna mambo mengi ya kuisadia jamii yanayopaswa  kufanywa huku ukiwa ndani ya mfumo uliosajiliwa rasmi.


Amewapongeza BRELA kuwa miongoni mwa watoa huduma kwenye maonesho hayo.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI