Takribani asalimia 70 ya vifo Duniani husababishwa na magonjwa yasiyoambukiza kutokana na mtindo wa maisha watu wengi wanaoishi.
Hayo yamebainishwa na Mratibu wa kituo Cha kuratibu Matukio ya dharura ya afya ya jamii Hospitali ya Sekouture Mkoani Mwanza Dr Nangi William na kueleza kuwa magonjwa Hayo yana madhara katika maisha ya binadamu hivyo hupelekea umasikini ndani ya jamii.
Nangi ameeleza kuwa ili kuondokana na magonjwa Hayo jamii inapswa kubadili mtindo wa maisha na kufata kanuni za afya Kama inavyoelekezwa na wataalamu ili kuweza kuwa na afya Bora na kuepukana na magonjwa hayo.
"Namna tulivyozoea kuishi na kula vyakula bila kufata mpangilio na kutoshughulisha mwili kwa kazi yeyote ndio maana tunasababisha magonjwa yasiyoambukiza kuongezeka" Alisema Nangi.
Nangi ameyataja baadhi ya magonjwa yasiyoambukiza yanayohatarisha maisha ya binadamu kuwa ni pamoja na ugonjwa wa moyo, Kansa, kisukari, saratani pamoja na tatizo la upumuaji .
Amefafanua kuwa Tafiti zimefanyika na kubaini vyanzo vinavyoweza kusababisha magonjwa Hayo ni pamoja na matumizi ya tumbaku, unywaji wa pombe kupitiliza, maisha bwete, aina ya vyakula vinavyotumika , uvutaji sigara pamoja na utumiaji wa ugoro.
"Ukiwa mgonjwa hauna muda wa kufanya shughuli za uzalishaji na badala yake unaangaika kutafuta Tiba ili uweze kurudi katika hali yako ya awali" Alisema Nangi.
Ameleza kuwa matumizi ya tumbaku na uvutaji wa sigara husababisha Kansa ya mapafu, unywaji wa pombe kupindukia husababisha sumu kuongezeka mwilini pamoja na kuishi maisha bwete.
"Ili tuweze kuepukana na magonjwa Hayo ni lazima ulaji wetu uwe mzuri na kupunguza ulaji wa sukari, mafuta, chumvi na kujishughulisha mwili Kwa kufanya mazoezi asubuhi na jioni Kwa kutembea na kukimbia Kwa kufanya hivyo mwili utachangamka na kutopata magonjwa yasiyoambukiza" Alisema Nangi.
Aidha ameeleza kuwa kutokana na Tanzania kuwa mwanachama wa shirika la Afya duniani hivyo kuelekea siku ya maadhimisho ya magonjwa yasiyoambukiza Kitaifa yatafanyika Mkoani Mwanza huku kauli mbiu ikisema Badili mtindo wa maisha kuwa na afya Bora.
0 Comments