VIJANA wa Visiwani Zanzibar wahimizwa kuchangamikia fursa ya kujiajiri wenyewe katika Sekta ya Kilimo cha Vanila pamoja na Vitunguu kwa lengo la kuondokana na Utegemezi na kujikwamua na Umasikini.
Wito huo umetolewa baadhi ya Vijana mbalimbali waliojitokeza katika Uwekezaji wa zao la Vanila pamoja na Vitunguu swaumu katika eneo la Bungi Mkoa wa Kusini Unguja ambapo wameeleza namna wanavcyonufaika katika kilimo cha Vanila pamoja na Vitunguu swaumu.
“Hapo awali nilikuwa nipo Maskani tuu, navuta bangi tu lakini kwasasa nimeamua kuwekeza katika kilimo hichi na sasa nanufaika hivyo nina washauri vijana wenzetu kuwaza kujitokeza,”ameeleza Mohameed Mzee.
Mohammed Mzee ameeleza kwamba, Kilimo hicho kina faida kubwa kutokana kuwa ni kilimo cha Muda mrefu na gharama zake za uendeshaji ni kidogo kulinganisha na kilimo kingine.
“Kilimo hichi unaweza kikistawi kinadumu kwa muda wa Miaka 60 unavuma tuu hivyo ni kilimo ambacho faida yake inadumu muda Mrefu sana,”ameeleza Mohammed Mzee.
Nae Kassim Kasilitano ameeleza namna muamko kutoka kwa Vijana wenziwe ndio uliompelekea kushiriki katika kilimo hicho ambapo kwa muda mfupi ameona mafanikio katika kilimo hicho.
Amesema kuwa Vijana wa Kizanzibar waache tabia ya kukaa vijiweni na kupiga story badala yake wanatakiwa kujitokeza katika Kilimo kwani kina fursa kubwa katika kuwainua kimaisha.
“Vijana wenzangu munatakiwa kuchangamkia fursa ya kilimo kina inainua maisha yetu na kutokuwa tegemezi,” alisema.
Kwa Upande wake Maneja Msaidizi wa Shamba la Vanila International Limited Twaha Mohammed ameeleza kwamba katika shamba hilo wameajiri vijana wengi kutoka Zanzibar na Tanzania bara hivyo vijana wengine wanapaswa kuchangamkia fursa hiyi.
“Kiukweli kuna fursa kubwa katika kilimo hivyo tuwakaribishe Vijana wote wa kuja kuwekeza na kulima mazao kama vile Vanilla, Vitunguu swaumu pamoja na Vitunguu maji na rangi rangi,” ameeleza.
0 Comments