Header Ads Widget

SERIKALI YATOLEA UFAFANUZI KUHUSU MSAMAHA WA TOZO

 

Na Fatma Ally Matukio Daima APP Dar es Salaam

Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango leo imetoa ufafanuzi kuhusu msamaha wa tozo uliotolewa September 20, na Waziri wa fedha na Mipango DKt Mwigulu Nchemba Bungeni Jijini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na majibu.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati akitoa ufafanuzi huo Kamishna Msaidizi Uchambuzi wa Sera Wizara ya Fedha na Mipango William Mhoja amesema kuwa Serikali imefuta tozo  kuanzia shill 0 hadi shill 30,000.


Amesema kuwa, katika ufutaji wa tozo na utoaji wa msamaha wa tozo hizo umezingatia hatua zote za kuwashirika wadau wakiwemo wamiliki wa mabenki na mitandao ya simu pamoja na kuangalia watumiaji wa kawaida wakiwepo wanachama wa Tasaf.


Aidha, amesema kuwa Serikali kuanzia Oct 1 mwaka huu itafuta na kusamehe tozo kuanzia asilimia 10 hadi 50, huku akibainisha kuwa utozaji wa tozo hizo si adhabu bali ni kwa ajili ya kuendesha Serikali.


"Serikali imepunguza wogo wa tozo, kuchochea matumizi ya miamala kwa ajili ya kupunguza fedha taslimu katika kurahisisha utozaji na kuzuia kutoza fedha mara mbili"amesema Mhoja .


Aidha, marekebisho yaliyofanyika ni kufuta tozo ya kuhamisha fedha kutoka benki kwenda mitandao ya simu pande (zote) na kufata tozo ya kuhamisha fedha ndani ya Benki, ambapo marekebisho mengine ni kufuta tozo ya kuhamisha fedha kutoka benki nyengine pande zote .


Hata hivyo, amesema pia Serikali imesamehe tozo ya miala kwenye utoaji wa fedha taslimu kupitia wa fedha kupitia wakala wa benki na ATM kwa miamala yenye thamani isiyozidi  shill 30,000, ambapo viwango vya tozo vilishushwa kwa asilimia 30 kutoka kiwango cha juu ch shill 10,000 hadi kiwango cha juu shill 7000.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI