Header Ads Widget

TBS WATOA ELIMU MAONYESHO YA 17 YA AFRIKA MASHARIKI JIJINI MWANZA.

 


Shirika la viwango nchini Tanzania ( TBS ) yawataka wananchi wa mkoa wa Mwanza pamoja na Kanda ya Ziwa kuthibitisha ubora wa bidhaa zao ili kutengeneza mnyororo wa thamani wa mazao ya kilimo na kupata fursa ya kuuza bidhaa zao ndani ya Jumuhiya ya afrika mashariki.



Rai hiyo imetolewa Jijini Mwanza na meneja wa Shirika hilo Kanda ya Ziwa Ismail Mwaipaya kwenye Maonyesho ya 17 ya wafanyabiashara ya Afrika Mashariki yanayofanyika katika Uwanja wa mpira wa Nyamagana Jiji humo.



Shirika la viwango Tanzania  ( TBS ) wanashiriki Maonyesho ya 17 ya Wafanyabiashara ya Afrika Mashariki Jijini Mwanza, lengo  likiwa ni kutoa elimu kwa wafanyabiashara ili kuthibitisha ubora wa bidhaa zao.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI