NA HAMIDA RAMADHAN MATUKIO DAIMA APP DODOMA
JUMLA ya Sh. Bilioni 1.2 zimetolewa na Benki ya Maendeleo ya kilimo Tanzania (TADB) kwa vikundi 10 vya wafugaji ili waweze kuongeza uzalishaji wa maziwa nchini.
Afisa Biashara Mkuu kutoka Benki hiyo ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Daniel Mwalyago alibainishwa hayo jijini hapa wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya unywaji maziwa mashuleni ambapo maadhimisho hayo kitaifa yalifanyika jijini Dodoma
“Katika kuazimisha siku ya unywaji maziwa shuleni tumefanikiwa kutoa mkopo wa sh.bilioni 1.2 kwa vikundi 10 vya wafugaji lengo la Benki ya TADB kutoa mikopo hii ni kwa ajili ya kuongeza uzalishaji wa maziwa nchini.
Alisema Kwanini wametoa fedha hizo kwa wafugaji hao ni baada kuona changamoto ambazo zimekuwa zikiwakumba wazalishaji wa maziwa nchini ikiwemo kupata mitamba isiyokidhi mahitaji ambapo Benki ya TADB imeweza kuwaletea mitamba ambayo inaweza kuongeza tija katika uzalishaji na kutoa maziwa mpaka lita 30.
" Niwatake wananchi na vikundi ambao wanajihusisha na usindikaji wa maziwa kufika katika benki ya maendeleo ya kilimo kwa ajili ya kupata utaratibu wa kujua jinsi gani wanaweza kufaidika na kupata mikopo kupitia sekta ya ufugaji," alisema
Aidha alisema wanakabiliwa na Changamoto kwa ng’ombe waliopo hawakidhi vigezo ambapo wafugaji wanazalisha maziwa lita mbili hadi saba.
"Lakini kwa mitamba hii mipya itasaidia kuongeza uzalishaji hadi kufikia lita 30 kwahiyo tunaamini tuitapaisha sekta ya maziwa hapa nchini," alisema
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Wafugaji kutoka Mkoa wa Tanga Beatrice Mseleu aliipongeza Benki ya TADB kwa kuwawesha kupata mkopo wa sh.milioni 243 ambao umesaidia kupata ng’ombe 52.
Alisema kikundi hicho kimeundwa na wanawake 10 ambapo kutokana na fedha hizo za mkopo walizopata wameweza kuongeza kiwango cha uzalishaji maziwa kwa asilimia 20.
“Tunaiomba Benki ya TADB iendelee kutuwezesha kupata vifaa kwa ajili ya kuchakata majani kwa ajili ya malisho ya mifugo ili kiwango cha uzalishaji kiongezeke zaidi ili kufikia adhima ya wataalamu wa afya ya kutaka kila mtu anywe lita 200 kwa mwaka,”alisema
Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Wafugaji kutoka Mbeya Anyelise Mwalukasa alisema chama chao wanakusanya maziwa zaidi ya lita 5,500 kwa siku.
Aliwashukuru benki ya TADB kwa kuweza kuwapatia mkopo kwa ajili ya kuongeza uzalishaji ambapo wamefanikiwa kupata mkopo wa sh.milioni 324.3 kwa ajili ya kununua ng’ombe 84.
“Hivi ninavyoongea tayari ng’ombe hao wamewasili nchini na tayari tumewakabidhi wanufaika ambapo kati ya ng’ombe 84 tulionunua 47 tayari wamezaa na tunategemea uzalishaji wa maziwa kuongezeka hadi kufikia lita 10,000 kwa siku
Aliongeza”Tunatoa wito kwa wafugaji wengine kwamba benki zinakopesha na sisi ni miongoni kati ya wanufaika ambao tumepata mkopo na tunaishukuru serikali kwa kuendelea kuwekeza katika benki ambayo imekuwa mkombozi kwa wananchi wanyonge.
0 Comments