NA TITUS MWOMBEKI, Matukio Daima App Kagera.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako amewataka viongozi katika Manispaa ya Bukoba kutoa mikopo kwa usawa katika makundi yote ili kusaidia makundi hayo kujikwamua kiuchumi.
Ameyasema hayo alipokuwa katika ziara maalumu ya siku mbili katika manispaa ya Bukoba mkoani Kagera na kutembelea vikundi vinne, kikundi cha Muungano Group kinachotengeneza vitafunwa, Maendeleo Pwani kinachojihusisha na shughuli za useremala, Kikundi cha Tuinuane, kikundi cha umoja mafundi kinachojihusisha na ushonaji wa suti pomoja na kava za magari, huku akiwataka viongozi kumpeleka katika vikundi vya watu wenye ulemavu atakaporudi katika ziara ya kilele cha kuzima mwenge inayotarajiwa kufanyika Oktoba 14 mwaka huu mkoani Kagera.
“Naishukuru halmashauri kwa kuweza kutoa mikopo kwa vijana,na niombe uhakikishe utoaji wa mikopo kwa makundi yote kwa usawa kama inavyotakiwa kwani hili ni suala la kisheria, asilimia mia nne kwa vijana, asilimia nne kwa wanawake na asilimia mbili kwa watu wenye ulemavu"
"kwa sababu nimeona vijana wanajitahidi kwa kutumia mikopo wanayoipata nilirudi hapa katika kilele cha mbio za mwenge nataka kutembelea vikundi vya watu wenye ulemavu ili nione nawao wanavyojikwamua kwa kutumia mikopo hiyo” Alisema Waziri Prof. Ndalichako.
Naye mwanachama wa kikundi cha Tuinuane, Mecktirda Jovinal wakati alisoma risala amewashukuru waziri Prf. Ndalichako pamoja na viongozi wa manispaa ya Bukoba kwa kuwapatia mikopo kwa ajiri ya kufanya shughuli za ujasiliamari huku akiomba kuwa nao bega kwa bega katika shughuli zao.
0 Comments