Header Ads Widget

DKT, PHILIP MPANGO KUWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA UJENZI CHANZO CHA MAJI BUTIMBA UTAKAO GHARIMU KIASI CHA BIL. 69.3 MKOANI MWANZA

NA CHAUSIKU SAID

MATUKIO DAIMA APP MWANZA.

Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, Philip Mpango anatarajia kuweka jiwe la msingi kwenye mradi wa ujenzi wa chanzo Cha maji Butimba utakaogharimu kiasi Cha sh, Bil 69.3 katika ziara yake ya siku tatu (3) anayotarajia kufanya Mkoani Mwanza.



Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Adamu Malima alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya ujio wa makamu wa Rais Mkoani hapa na kueleza kuwa mradi huo utazalisha lita Mil,48 kwa siku utasaidia uboreshaji wa huduma ya upatikanaji wa maji Safi kwa wakazi wapatao laki nne na nusu (450,000) Jijini hapa.


Malima amesema kuwa mradi huo unao simamiwa na mamlaka ya maji Safi na usafi wa mazingira Mwanza ( MWAUWASA) utekelezaji wake umefikia Asilimia 40 na unategemewa kukamilika mwezi februari 2023.


Malima ameeleza kuwa Makamu wa Rais pia atazindua jengo la Mama na Mtoto katika hospital rufaa ya Mkoa wa Mwanza sekou toure lenye thamani ya sh Bil.10.1 ambapo mradi huo utaboresha huduma ya afya kwa wananchi hususani kwa Mama na Mtoto.


Ameeleza kuwa jengo Hilo litapunguza msongamano kwa wagonjwa uliopo kwa sasa na kutoa huduma kwa vitanda 261 na kupunguza vifo vya Mama na Mtoto wakati wa kujifungua.


Kwa upande mwingine ameeleza kuwa katika halmashauri ya ilemela atazindua stendi ya kisasa ya mabasi na Maegesho ya malori ya Nyamohongolo yenye thamani ya Bil. 26.6.


Malima amesema kuwa stendi hiyo utasaidia kuongeza mapato ya Halmashauri na kuvutia wawekezaji na kuongeza idadi  ya wafanyabiashara ndani ya Halmashauri ya manispaa ya Ilemela pamoja na kuboresha usafiri na usafitishaji wa abiria.


Aidha amefafanua kuwa mradi huo unakadriwa kukusanya sh, Bil. 2.2  kwa mwaka pamoja na kuongezeka kwa fursa za Ajira taktibani 1300.


Aidha ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kumpokea Makamu wa Rais .

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI