Header Ads Widget

MWANAMKE ANAPASWA KUNYWA BIA MOJA KWA SIKU NA MWANAUME BIA 2 ILI KUEPUKA MAGONJWA HAYA..

 


Mwenyekiti wa Shirikisho la Magonjwa yasiyo ya Kuambukiza Tanzania, Profesa Andrew Swai amesema mwanaume anatakiwa kunywa chupa mbili za bia kwa siku ili ajiweke salama dhidi ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza huku mwanamke akitakiwa kunywa chupa moja.

Profesa Swai amebainisha hayo leo Alhamisi, Septemba 29, 2022 wakati akizungumza na kituo kimoja cha redio kuhusu Siku ya Moyo Duniani ambapo amebainisha unywaji sahihi wa pombe kwa viwango visivyo hatarishi.

Amesema glasi moja ya mvinyo ni sawa na chupa moja ya bia wakati shoti mbili za pombe kali ni sawa na chupa moja ya bia.

“Mwanaume mtu mzima unatakiwa usizidishe chupa mbili za bia na mwanamke usizidishe chupa moja ya bia kwa siku,” amesema Profesa Swai ambaye pia ni mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala.

Profesa Swai amesema mtu anapozidisha kiwango hicho, ini linaumia zaidi kutokana na kiwango cha sumu kinachongia mwilini.

Hata hivyo, amesema athari zinajitokeza kulingana na uimara wa mtu na mtu katika kuhimili sumu hizo, amesema kwa baadhi ya watu athari hizo zinachelewa kujitokeza wakati wengine zinawahi:Chanzo Mwananchi 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI