Hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan alitoa wito kwa idara zinazohusiana na upelelezi kuhakikisha kwamba wanafanya upelelezi na kuwa na ushahidi wa kutosha kabla ya kumkamata mtuhumiwa na kumweka mahabusu .Akizungumza mara baada ya kuwaapisha rasmi Majaji Mei 17, 2021 jijini Dar es Salaam, Rais Samia alisema kuwa “Tatizo la ucheleweshwaji wa kesi katika Mahakama zetu bado lipo, kama mnavyosema Wanasheria haki inayocheleweshwa ndio haki inayokataliwa, hivyo ni imani yangu kuwa baada ya upatikanaji wa Majaji hawa ucheleweshaji wa kesi Mahakamani utapungua na hatimaye haki kupatikana kwa wakati,” Aidha, Mhe. Rais aliviagiza vyombo vya upelelezi nchini kufanya kazi zake za upelelezi kwa wakati ili kuwezesha kesi kumalizika kwa wakati ili wananchi waweze kupata haki zao kwa muda muafaka” https://www.judiciary.go.tz/web/index.php?r=posts%2Fwebview&id=413
Licha ya kauli hii ya Rais ya kuzingatia heshima, hifadhi na ulinzi wa Haki za Binadamu lakini bado kumekuwepo na changamoto ya utekelezaji wake kwa ofisi na idara za umma zinazohusika (Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka ) ambaye anatakiwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 59B (4) (a) ,(b) kuzingatia nia ya kutenda Haki na kuzuia matumizi mabaya ya taratibu za utoaji wa Haki.Pia kauli ya Rais inalenga kuhakikisha kwamba watuhumiwa wanapata haki zao kama inavyoelezwa kwenye Ibara ya 107A (2) (b) kuhusu Mahakama kutochelewesha haki bila sababu ya kimsingi.
Hivyo Shirika la Civic and Legal Aid (CILAO) kwa kushirikiana na wadau wa Haki za Binadamu nchini tunakusudia kukusanya taarifa ya kesi zilizoko mahakamani kwa muda mrefu bila kusikilizwa kwa kile kinachoelezwa kwamba upelelezi haujakamilika.
Lengo likiwa ni kuunga mkono kauli na juhudi za Rais na Kusukuma utekelezaji wa kauli yake ili kuhakikisha upatikanaji wa Haki kwa wakati.
0 Comments