Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2022 Sahili Geraruma amepongeza shughuli zinazofanywa na Manispaa ya Sumbawanga ikiwemo usimamizi na utekelezaji wa miradi.
Geraruma ametoa pongezi hizo leo (21.09.2022) wakati akikagua miradi iliyotembelewa na Mwenge wa Uhuru ikiwemo shule ya msingi Kakwale na kikundi cha Vijana wajasiliamali .
Kiongozi huyo alisema alisema mradi wa madarasa mapya matatu Shule ya Msingi Kikwale ni mazuri lakini yalichelewa kukamilika ambapo yamegharimu Shilingi Milioni Sitini.
" Mradi huu ni mzuri na umelengwa kwa ajili ya kunufaisha wanafunzi kusoma kwenye mazingira bora. Hata hivyo kasoro tulizoona ni wataalam kutekeleza mradi huu kwa kuchelewa bila sababu za msingi" alisema Geraruma.
Mwenge wa Uhuru umefanikiwa kuweka jiwe la msingi la mradi ujenzi wa madarasa ya Elimu ya Watu Wazima, Jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya Tawaqal- Mahakama Kuu na kutoa mikopo kwa vijana wajasiliamali yenye thamani ya Shilingi Milioni 10.
Ukiwa Manispaa ya Sumbawanga Mwenge wa Uhuru umekagua miradi mitano yenye thamani ya Shilingi Bilioni Moja na Milioni Mia Nane huku ukikimbizwa umbali wa kilometa 97.
Kesho Mwenge wa Uhuru utaendelea na Mbio zake kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi.
Mwisho.
0 Comments