Header Ads Widget

KIONGOZI MBIO ZA MWENGE ASHANGAZWA NA MAPIGANO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI

 


Na Fadhili Abdallah,Kigoma


KIONGOZI wa mbio za mwenge wa uhuru kwa mwaka huu Sahel Geraruma  amewataka wananchi wa wilaya ya Kigoma kujitokeza kwa wingi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo badala ya kuwa sehemu ya migogoro inayosababisha mauaji kwenye jamii.


Akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi wa maji kwenye kijiji cha Pamila halmashauri ya wilaya Kigoma kiongozi huyo wa mbio za mwenge alisema kuwa ugomvi na mapigano hasa ya wakulima na wafugaji ni adui mkubwa wa maendeleo.


Alisema kuwa hakuna sababu ya watu kushikiana mapanga na mikuki na kusababisha mauaji bali watu wote wajenge upendo,amani na mshikamano miongoni mwao na kazi yao iwe moja kumuunga mkono Raisi Samia Suluhu Hassan katika kuleta maendeleo.


Awali akizungumza katika uzinduzi wa mradi huo Mbunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini,Asa Makanika alisema kuwa pamoja na kuzinduliwa kwa mradi mkubwa wa maji katika kijiji hicho lakini kuna mgogoro mkubwa baina ya wakulima na wafugaji na mamlaka za serikali zinajua jambo hilo.


Makanika alisema kuwa migogoro hiyo imekuwa adui mkubwa wa maendeleo kwa wananchi wa kijiji hicho kwani imesababisha chuki  baina yao.


Akitoa taarifa ya mradi huo wa maji Mhandisi wa Maji wa wakala wa maji mijini na vijijini (RUWASA) wilaya ya Kigoma, Leon Mwombeki alisema kuwa kiasi cha shilingi milioni 580.6 kimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo ambao kwa sasa umefikia asilimia 95.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI