MKuu wa Kikosi Cha usalama barabarani mkoa wa Iringa (RTO) Mosi Ndozero akiagiza Madereva wawili wa Mabasi ya abiria ya Iringa -Mafinga kupigwa pingu na kuwekwa mahabusu leo Katika stendi kuu ya Mabasi ya Igumbilo Iringa baada ya kuvunja sheria za usalama barabarani.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa Allan Bukumbi akiwasili eneo la milima Kitonga Kukagua na kutoa elimu ya usalama barabarani Kwa Madereva Leo Mkuu wa Trafiki mkoa wa Iringa Mosi Ndozero akiwa kazini leo
Mkuu wa usalama barabarani mkoa wa Iringa Mosi Ndozero akitoa elimu Kwa Madereva eneo la stendi ya Igumbilo
JESHI la Polisi mkoa wa Iringa limefanya oparesheni maalum iliyoambatana na utoaji elimu ya usalama barabarani Kwa Madereva wanaotumia barabara kuu ya Iringa-Dar es Salaam.
Zoezi hilo limeongozwa na Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Iringa RPC Alan Bukumbi na mkuu wa Kikosi Cha usalama mkoa wa Iringa RTO Mosi Ndozero .
Kamanda wa Polisi wa mkoa Iringa Allan Bukumbi amewataka Madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani na kuwa hatua Kali zitachukuliwa Kwa wote wanaovunja sheria za usalama barabarani .
Akizungumza Katika oparesheni hiyo mkuu wa Trafiki mkoa wa Iringa Mosi Ndozero amesema kuwa elimu hiyo itasaidia kupunguza .
HABARI ZAIDI KUPITIA TAARIFA YA HABARI YA MATUKIO DAIMA TV SAA MOJA USIKU WA LEO
0 Comments