Header Ads Widget

WATUMISHI WATAKIWA KWENDA KUWAELIMISHA WANANCHI JUU YA UHIFADHI WA MAZINGIRA

 



Na Gift Mongi _Moshi


Taasisi zinazohusika na usimamizi wa rasilimali ya maji ikiwemo mamlaka ya maji bonde la Pangani zimetakiwa kutoka ofisini na kwenda kuwaelimisha wananchi umuhimu wa kutunza mazingira.


Hali kadhalika katika kukutana na wananchi hao itaenda kuwa ni mojawapo na kukutana na njia ambazo zimekuwa zikiathiri vyanzo vya maji hivyo kuwa rahisi kuweza kudhibiti uharibifu.


Akizungumza mbele ya waziri wa maji Jumaa Aweso mbunge wa Moshi Vijijini Prof Patrick Ndakidemi alisema wataalam wengi wamekuwa wakikaa ofisini badala ya kutoka na kukutana na watumia maji ili kujua kero zao na njia sahihi ya kuzitatua.


"Yaani wanabaki ofisini badala ya kwenda kuwatembelea wale ambao ndio watumia maji lakini ndio waangalizi wa vyanzo vya maji ni lazima waende waelimishwe njia sahihi katika uhifadhi mazingira"alisema Prof Ndakidemi


Kwa mujibu wa Prof Ndakidemi ni kuwa wananchi ndio wenye vyanzo hivyo na kuwa  wakipewa elimu wataweza kuwa ni walinzi wazuri kwani kwa sasa huenda wanafanya uharibifu bila wao wenyewe kujua kutokana na uelewa duni walio nao


Kwa upande waziri wa maji Jumaa Aweso alisema watumishi waliopo kwenye idara mbalimbali ndani ya wizara hiyo wanatakiwa kubadilika na kuachana na kufanya kazi kimazoea


"Ni lazima tubadilike tuachane na ile dhana ya kufanya kazi kimazoea tutoke tukasikilize wananachi wana shida gani na tuone namna ambavyo tunaenda kuziletea ufumbuzi"alisema


Alisema ameridhishwa na utekelezaji wa miradi mbali mbali kwa mkoa wa Kilimanjaro inavyokwenda na kuwa dhamira ya awamu ya sita na kuhakikisha maji yanapatikana na kumaliza kero za muda mrefu.


"Nimeshuhudia miradi inavyokwenda kwa mkoa niwapongeze ila muongeze kasi katika usimamizi wa miradi hii ili iweze kukamilika kwa wakati kama ambavyo ni malengo ya serikali yetu"alisema


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI