Kupitia majibu ya Pingamizi aliyowasilisha, Rais Mteule amesema Mahakama Kuu haitakuwa na Mamlaka ya kumtangaza Odinga kuwa Rais hata baada ya kujumlisha Kura na kuthibitisha Matokeo kama ilivyoombwa
Ameongeza kuwa maombi ya Odinga na mgombea mwenza wake, Martha Karua, ni kinyume cha #Katiba na kwamba Kiongozi huyo wa Azimio amedhamiria kulazimisha ushindi ili wagawane Mamlaka
Ruto amenukuliwa akisema “Ni Pingamizi potofu, wao wanadai kuwa hakuna Mgombea aliyefikia 50% ya Kura na kwa vyovyote vile, Kifungu cha 80 (4) cha Sheria ya Uchaguzi kinaizuia Mahakama hii Tukufu kutoa uamuzi wa Malalamiko kwasababu waombaji walitenda makosa ya Uchaguzi,”.
0 Comments