Header Ads Widget

DKT NDUMBARO AWATAKA MADIWANI WA SONGEA MJINI KUFANYA MIKUTANO YA HADHARA NA WANANCHI

  


Na Amon Mtega, MatukioDaimaAPP,Ruvuma 

MBUNGE wa Jimbo la Songea Mjini Dkt Damas Ndumbaro ambaye pia ni Waziri wa Katiba na Sheria amewataka madiwani wa Manispaa ya Songea kufanya mikutano ya hadhara na Wananchi ili kubaini changamoto zinazowakabili Wananchi hao  kisha kuzitatua kwa haraka.


Dkt Ndumbaro ameutoa wito wakati akitoa salamu za kibunge kwenye kikao cha kawaida cha baraza la Madiwani la robo ya nne ya mwaka ambapo agenda mbalimbali zimejadiliwa ikiwemo na kusimamia suala la ruzuku ya mbolea iliyoweka na Serikali.


Mbunge Dkt Ndumbaro amesema kuwa madiwani wakijenga utamaduni wa kufanya mikutano ya hadhara ya mara kwa mara kwenye kata zao kutaendelea  kutawajengea Imani Wananchi yakutatuliwa kwa changamoto zao.



 Amefafanua kuwa kumekuwepo kwa baadhi ya malalamiko kutoka kwa Wananchi ambayo yanahitaji ufafanuzi wa Viongozi husika lakini hayafafanuliwi kwa wakati ni kutokana na baadhi yenu madiwani kutokufanya mikutano na Wananchi.


Katika hatua nyingine Mbunge Dkt Ndumbaro amesema kuwa yeye ni mbunge wa kufanya kazi za kuwaletea maendeleo wananchi na siyo kusikiliza maneno ya majungu ya watu wanayoyazungumza juu ya ufanyaji kazi.


 "Nilazima tufanye kazi za Wananchi walizotutuma na siyo vinginevyo hivyo ni vema kila Diwani aone anawajibu wa kulipa deni la Wananchi kwa kuwafanyia kazi"amesema Dkt Ndumbaro.


 Hata hivyo Mbunge huyo amempongeza mkurungenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Dkt Fredrick Sagamiko kwa kusimamia vema zoezi la Sensa ambalo kwa Manispaa hiyo limeenda vizuri bila changamoto za kutisha kama zinazosikika kwenye baadhi ya maeneo mengine.


 Naye mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Songea Mjini Hamis Abdallah Ali wakati akitoa salamu za chama hicho alipokuwa amealikwa kwenye baraza hilo amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imeshaweka ruzuku ya sh.60,000  kwenye kila mfuko wa mbolea hivyo Chama cha Mapinduzi kinawaomba maafisa ugani kwenda  kusimamia zoezi hilo kikamilifu ili kusitokee malalamiko kwa Wananchi ambao wengi wao ni wakulima.


Kwa upande wake meya wa Manispaa ya Songea Michael Mbano wakati akipokea salamu hizo amesema kuwa ataenda kuzifanyia kazi kwa kuzitekeleza ikiwemo ya kuhakikisha madiwani wanafanya mikutano ya hadhara na Wananchi pamoja na kumuhimiza mkurungenzi wake kuwasimamia maafisa ugani kwenda kuwahudumia Wananchi ambao ni wakulima .






      

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI