Header Ads Widget

VIFAA TIBA VYENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 112 VIMETOLEWA KWA AJILI YA UCHUNGUZI KATIKA WILAYA ZA BIHARAMLO NA MULEBA MKOANI KAGERA.


Na Shemsa Mussa-Matukio Daima 

Kagera.

Shirika la Afya Duniani  WHO kwa kushirikiana na wizara ya Afya wamekabidhi vifaa Tiba katika serikali ya Mkoa Kagera  Ambavyo vitafanya uchunguzi kwa wagonjwa katika Halmashauri za  Biharamulo na Muleba  vyenye Thamani ya shilingi Milioni 112 kama sehemu ya kurejesha hali tangu Mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya Marbug Ulipotokea .

Mkurugenzi Mkazi wa mwakilishi wa  shirika la   Afya Duniani Dr Galberth  Fadjo amesema kuwa  shirika Hilo limekuwa na jitihada za Serikali kupitia wizara ya Afya Tanzania kwa namna linavyochukua hatua za haraka juu ya kudhibiti magonjwa yenye nguvu yasisambae zaidi na kuhakikisha wanaopata madhara au  ugonjwa  wanarudi katika hali zao haraka bila kuleta madhara.

"Mfano wa mlipuko wa ugonjwa wa Marbug  katika huu mkoa wa Kagera wilaya ya Bukoba  mwaka 2023 na wilaya ya Biharamulo mwaka  2024 namna serikali ilivyopambana bila kuathiri shughuli nyingine na   wakaweza kurejesha hali katika jamii ,hii inatakiwa kuwa ni mfano wa kuigwa kwa nchi nyingine zinazokabiliana na Majanga ya magonjwa hatari ya mlipuko kama hayo,amesema Bw Fadjo"


Amesema WHO itaendelea kukabiliana na dharura kwa uharaka katika kupambana na magonjwa ya mlipuko  huku akitoa wito kwa mamlaka kutumia vifaa hivyo kutoa elimu ya kiutaalamu kwa watakaovitumia na kuendelea kuweka mazingira mazuri ya kupambana na magonjwa ya mlipuko .

Mkurugenzi wa dharura na maafa kutoka wizara ya Afya Dr.Erasto Sylvanus amesema  kuwa vifaa vilivyopokelewa  ni vitanda vya kisasa vya kulaza wagonjwa,machine za kusafisha mashuka,stendi za kuwekea dawa,ndoo za kuhifadhi maji na Kufanyia usafi katika vituo vya afya pamoja na vifaa  vya kufanya uchunguzi wa kina.

Amesema  ugonjwa huo umewapa Mafunzo mbalimbali ambapo wizara ya Afya imejifunza  kutoa elimu kwa wananchi kutoa taaarifa ya dharura  pale wanapoona ugonjwa usio wa kawaida, kuimarisha utayari ,kushirikisha jamii pamoja na kuunganisha Wadau katika kudhibiti 

Dr Sylvanus,Amesema kuwa vifaa vilivyotolewa vitaongeza ujuzi na utendaji kazi kwa wataalamu wa afya mkoani Kagera ambapo amelishuru shirika la WHO kwa utayari na usaidizi mzuri wa katika kipindi chote ambacho nchi ya Tanzania na mkoa wa Kagera walipokumbwa na mlipuko Wa ugonjwa huo.



Ametoa wito kwa halmashauri za mkoa wa Kagera kutenga bajeti ya ndani kwa ajili ya kukabiliana na Magonjwa ya mlipuko yanayojitokeza kwa dharura na kudai kuwa Mpaka sasa tayari wamekuwa na uzoefu juu ya magonjwa mbalimbali ya mlipuko.

Naye Katibu tawala wa mkoa wa Kagera  Steven Ndaki ametoa wito kwa wataalamu kuvitunza vifaa hivyo  vilivyotolewa na  kuongeza ujuzi  wa kuvitumia pamoja na kuendelea kutoa taarifa kwa wananchi juu ya kujikinga na ugonjwa huo bila kujali   kama Kuna ugonjwa au hakuna ugonjwa 

Amesema mkoa wa Kagera utaendelea kujiweka  tayari kwa ajili ya kukabiliana na dharura  Zote za mlipuko kutokana na mkoa huo kupakana na  nchi nyingi ambazo zinaongeza uhatarishi wa magonjwa ya mlipuko.


 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI