Header Ads Widget

WATANZANIA WATAKIWA KULA KOROSHO KWA WINGI ILI KUIMARISHA AFYA ZAO



NA HADIJA OMARY, LINDI.


WATANZANIA wametakiwa kula Korosho kwa Wingi ili kuimarisha Afya zao na kukuza soko la ndani litakalopelekea ukuwaji uchumi wa Taifa.


Wito huo Umetolewa na Mkuu wa mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abasi katika tukio maalumu la kula na kunywa Korosho lililoandaliwa Bodi ya Korosho Tanzania kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo TARI kituo cha Naliendele lililofanyika katika viwanja vya maonyesho ya Wakulima (nane nane)Ngongo Manispaa ya Lindi Mkoani humo.



Kanali Ahamed alisema kuwa ulaji wa Korosho zinazozalishwa hapa Nchini, pamoja na kuimarisha Afya za Wananchi inasaidia kuongeaza na kuimarisha Soko la ndani la korosho na Bidhaa zake.


Alisema kupitia ongezeko la ulaji wa Korosho  utaweza kuhamasisha wajasiliamali na wawekezaji kujikita katika kuongeza Mnyororo wa Thamani katika Zao la Korosho.



Mnyororo wa thamani katika zao la Korosho utasaidia kuchochea ukuwaji wa viwanda vya hapa Nchini ambavyo vitazalisha bidhaa zilizoongezwa Thamani na kuuza hata nje ya Nchi kwa bei ya kimataifa na kujipatia fedha nyingi za kigeni.


Hata hivyo kanali Ahmed aliongeza kuwa kutokana na ongezeko la mahitaji ya Korosho na Bidhaa zake kupitia hamasa ya siku ya ulaji wa Korosho Nchini aliwaomba Bodi ya Korosho na TARI – Naliendele kuhakikisha kuwa siku ya ulaji wa Korosho ifanyike kila Mwaka.


Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Tanzania alisema kuwa Siku hiyo ya ulaji na unywaji wa Korosho ni muhimu sana kwa ajili ya kuongeza hamasa ya ulaji wa Korosho zinazozalishwa hapa Nchini.



Alisema ulaji wa Korosho na Mabibo pamoja na Bidhaa zake zitokanazo na korosho na mabibo zinafaida sana kwa Afya ya Binadamu.


“ Mfano Maziwa ya Korosho na Siagi hutupatia virutubisho vya Protini, Wanga na Mafuta kwa wingi , lakini pia hutupatia madini joto ya Chuma, magniziam na kopa ambayo huimarisha Mifupa sambamba na kuzalisha seri kwa wingi”.

 

“Mabibo ya korosho na Bidhaa zake hutupatia Vitamini C kwa wingi mara tano ya Vitamini C inayopatikana kwenye Machungwa ambayo inasaidia kulinda Mwili ”.


Nae mratibu wa Utafiti na ubunifu kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo TARI Kituo cha Naliendele , Dr. Geradina Mzena alisema kuongeza uzalishaji wa korosho hapa Nchini Taasisi yao imejipanga kuongeza nguvu katika utafiti sambamba na kuongeza uzalishaji bora wa Mbegu za Korosho kutoka tani 138 za sasa mpaka kufikia Tani 200 ambazo zitaenda kukidhi mahitaji ya mbegu bora za Korosho zinazohitajika Ndani na Nje ya Nchi.


Nae Kaimu Meneja Idara ya Uchumi  Aristedes Mrewa Alisema Zao la Korosho ni miongoni mwa mazao ya Biashara yanayoongoza kuipatia Nchi fedha za kigeni ambapo katika miaka ya hivi karibuni Serikali imeingiza fedha za kigeni milioni 220 mpaka 500 hivyo ili kuendelea kupata Fedha nyingi Zaidi ni muhimu kwa wananchi kuendelea kuwekeza katika zao hilo.


“Kwa hivyo sisi kama Benk kuu tunaliona zao la Korosho kama ni zao la kimkakati na tunaendelea kushauri wananchi waendelee kushiriki katika kurendeleza Zao hili kwani litakuwa na manufaa makubwa kwa kuongeza kipato kwa Mwananchi Moja mmoja  pamoja na kuongeza Fedha za kigeni”.


MWISHOOOO

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI