Na Amon Mtega_ Mbinga.
KATIBU wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma Jacob Siay amewapongeza wanachama na wapenzi wa CCM Wilayani humo kwa kujitokeza kushiriki changuzi za kuwapata Viongozi kwenye chama hicho toka Mashina,Matawi na Kata .
Pongezi hizo amezitoa wakati akizungumzia mchakato mzima wa uchaguzi wa CCM na Jumuiya zake kwenye Wilaya hiyo toka ngazi ya shina hadi kata na watamalizia na Wilaya.
Siay amesema kuwa Wilaya hiyo yenye kata 48 Matawi 313 na Mashina 2026 uchaguzi umefanyika na baadhi ya maeneo yaliyonyesha kuwa na changamoto mbalimbali yaliweza kufanyiwa utatuzi wa haraka na kuwafanya wanaccm kuendelea na uchaguzi wa kuwapata Viongozi wao.
Aidha katika hatua nyingine katibu huyo amewataka Viongozi waliyochaguliwa na wanaccm hao kwenye nafasi mbalimbali za Jumuiya na Chama wakashirikiane kuhakikisha wanatekeleza matakwa ya Chama ili jamii ikanufaike na utawala wa CCM na kuendelea kukiamini Chama hicho kuongoza Dola.
Hata hivyo ametumia nafasi hiyo ya kuwataka Viongozi hao pamoja na wanaccm wote katika Wilaya hiyo kuwa mstari wa mbele kuhamasisha wananchi kuhesabiwa Sensa Agosti 23 mwaka huu ili kuendana sambamba na mpango wa Serikali wa kupata takwimu sahihi ya Wananchi wake kisha kuendelea kuwaletea maendeleo.
0 Comments