Na Gabriel Kilamlya MBEYA
Wakati maonesho ya wakulima nane nane yakitarajiwa kuhitimishwa agosti 8 mwaka huu wataalamu wa kilimo nchini wametakiwa kuhakikisha wanawapa mbinu za kilimo cha kisasa kinachoendana na soko la ushindani katika mazao yao.
Katibu tawala mkoa wa Ruvuma Stephen Ndaki ametoa rai hiyo baada ya kutembelea banda la Halmashauri ya wilaya ya Wanging'ombe katika maonesho ya wakulima yanayofanyika kitaifa jijini Mbeya ambapo amesema wataalamu hao ni nafasi yao katika kipindi hiki kuwafikia wakulima wengi na kuwapa utaalamu stahiki kupitia maonesho hayo.
Christopher Mdakule ni miongoni mwa wakulima waliofika katika banda la Wanging'ombe kupata utaalamu huo na shauku yake ni kutaka kujifunza zaidi katika kilimo cha alizeti.
Afisa kilimo mifugo na Uvuvi Halmashauri ya wilaya ya Wangong'ombe Bernadetha Fivawo anasema wameendelea kutoa elimu kwa wakulima juu ya kulima kilimo chenye tija badala ya kutumia nguvu kubwa kulima eneo kubwa lisilo na tija.
Bernadetha anasema Hamasa imekuwa kubwa katika maonesho hayo ya wakulima katika siku za mwisho tofauti na walivyokuwa wanaanza.
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajia kufunga maonesho haya yanayotamatika Agosti 8,2022.
0 Comments