Header Ads Widget

WAKULIMA WA PAMBA WAHIMIZWA KUONGEZA UZALISHAJI.

 


Na Bahati Sonda, Simiyu.

Wakulima wa pamba hapa nchini  wamehimizwa kuongeza uzalishaji wa zao hilo ili kuendelea kutoa fursa za ajira kwa watu wengine kupitia kuzalisha bidhaa mbalimbali zinazoweza kuzalishwa kutokana na zao hilo ikiwemo mafuta ya kula sabuni na chakula cha mifugo.


Imeelezwa kuwa uzalishaji wa bidhaa hizo zitokanazo na mbegu za pamba upo chini kutokana na uzalishaji wa zao hilo kuwa mdogo hali inayopelekea mbegu nyingi zaidi kutumika kwenye upandaji na kwamba katika kukabiliana na changamoto hiyo na kuongeza tija na uzalishaji wa bidhaa hizo bodi ya pamba imeendelea na juhudi za kutoa elimu kwa wakulima wa zao hilo.



Akizungumza na wakulima wa zao hilo katika viwanja vya maonesho ya sherehe za wakulima nane nane Nyakabindi mjini Bariadi Afisa Kilimo Mkuu bodi ya pamba Emmanuel Kileo  ameeleza mnyororo mzima wa thamani wa zao la pamba mbali na bidhaa ya nguo inayotokana na zao la pamba mbegu za pamba pia hutumika kama malighafi ya kutengeneza bidhaa mbalimbali.


Aidha Kileo ameongeza kuwa bidhaa zinazotokana na mbegu za pamba hazizalishwi kwa wingi kutokana na uzalishaji wa pamba kuwa chini hali inayofanya mbegu zinazopatikana kutumika kwa ajili ya kupanda kutokana na tija ndogo wanayopata wakulima.



Katika hatua nyingine Said Itaso ambaye ni Mkaguzi wa pamba mkoani Simiyu amesema kuwa kuna mikakati ya kuongeza tija katika zao hilo na kwamba bodi hiyo itahakikisha mkulima anatumia teknolojia bora za kilimo.


Naye mkaguzi wa zao hilo Azaria Sanga ameeleza kuwa matumizi ya mbolea hususan samadi na palizi sahihi ni miongoni mwa mambo ya kitaalam yanayotakiwa kuzingatiwa na mkulima ili kupata mavuno mengi.


Hata hivyo wakulima waliopata elimu hiyo wamekiri kuwa awali hawakujua na elimu hiyo akiwemo Samwel Maduhu amebainisha kuwa walikuwa wakikosea maelekezo ya utumiaji na uchanganyaji wa sumu ya kuua wadudu na kusababisha kupata mavuno kidogo kidogo yasiyo.


Maduhu amekiri kuwa hawakuwa wanazingatia njia sahihi ya upuliziaji wa sumu ya kuua wadudu na kuelekeza malalamiko kwa bodi na kuishukuru kwa kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kwani wengi wao hawajui matumizi sahihi ya sumu hizo za kuuliza wadudu waharibifu wa zao la pamba.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI