Header Ads Widget

WAKULIMA MKOANI SIMIYU WAELEZA KUTOONA UMUHIMU WA ZANA ZA KILIMO

 


 Na Bahati Sonda, Simiyu.

Baadhi ya wakulima mkoani Simiyu wameeleza kutoona manufaa ya zana  zinazobuniwa na wabunifu hapa nchini kwa ajili ya kurahisisha shughuli zao za kilimo kutokana na zana hizo kuwa ghari hali inayofanya wengi kushindwa kumudu.


Wakulima hao wameyasema hayo baada ya kuzunguka na kujionea zana mbalimbali ambazo zimeletwa kwenye maonesho ya sherehe za wakulima marufu kama nanenane Kanda ya ziwa Mashariki yanayojumuisha Shinyanga , Mara na Simiyu ambao ndiyo wenyeji wake yanayofanyika katika viwanja vya Nyakabindi mjini Bariadi.



Wamebainisha kuwa tofauti na miaka iliyopita ambapo walitegemea zana toka nje ya nchi ili kurahishisha shughuli zake za shamba miaka ya hivi karibuni kumekua na mwamko mkubwa wa taasisi na watu binafsi kubuni zana mbalimbali za kilimo na kwamba maonesho ya wakulima huwapa fursa wakulima kujionea zana hizo.


Fadhili Makingi ni miongoni mwa wakulima waliofika katika viwanja vya nyakabindi na kujionea zana za kupandia pamba na mazao mengine pamoja na za kupalilia ambapo mbali na kukiri kuwa zina msaada mkubwa kwao ameeleza kuwa ameshindwa na kunufaika nazo kutokona na gharama yake kuwa kubwa kuliko uwezo wao.



Aidha Makingi ameiomba serikali 

"Mashine zilizopo ni nzuri na zina uwezo wa kumsaidia mkulima tatizo gharama zipo juu hivyo tunaiomba serikali ione ni namna gani inaweza kutusaidia kupata hizi zana kwa bei rahisi kwa kupitia mifumo iliyopo hususan ziwepo katika benki ya kilimo" Amesema Makingi


Kwa upande wake Donald Mtipa ambaye  ni Mtafiti wa magonjwa ya zao la pamba amekiri kuwa zana hizo zinamuwezesha mkulima kufanya kazi zake kwa urahisi kuliko kutumia nguvu kazi ya watu huku akiwashauri kutumia mbegu bora zitazowawesha kupata tija.

 

Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI