Na Rehema Abraham
Mbunge wa Jimbo la Moshi vijijin prof.Mh, Patrick Ndakidemi amewataka vijana Mkoani Kilimanjaro kujikita katika kulima kilimo Cha mazao ya biashara ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Prof.Ndakidemi amesema hayo wakati alipokuwa akizungumza katika kongamano la vijana la kuwahamasisha kujikita katika kilimo biashara iliyofanyika mkoani Kilimanjaro.
Aidha amesema kuwa Wizara ya kilimo imetenga Fedha Fedha ya kuwasaidia vijana waliojikita katika kilimo,na kusema ni vyema vijana wakajiunga katika vikundi ili waweze kupatiwa fedha hizo na waweze kuondokana na tatizo la umasikini.
"Vijana ambao wameamua kufanya sekta ya kilimo kama ajira na kulima kwa mfumo wa kilimo biashara, wamekiri kupata mafanikio makubwa tofauti na ajira ambazo walikuwa nazo hapo awali"Alisema prof.Ndakidemi.
Sambamba na hayo ameipongeza kanisa la KKKT kupitia shirika la Norwegian church aid kwa kuwaleta vijana hao pamoja ili waweze kuelezea mambo mbalimbali ya kimaendeleo wanazofanya na kusema jambo Hilo ni muhimu na lina Maendeleo kwa Taifa.
Amewataka pia vijana kujitambua na kujua thamani walizonazo kwani wao ndio Taifa la Leo na Taifa la Kesho ambapo amesema vijana walio wengi hawajielewi hivyo amewataka kujitambua hata kama hawana ajira lakini wanaweza kujiiingiza katika fursa za kilimo.
Hata hivyo amesema Kama vijana watatumia karama walizonazo na kujingiza kwenye ujasiriamali wataaweza kufanikiwa bila kutegemea kuajiriwa mahali popote.
0 Comments