Na Gabriel Kilamlya ,Matukio DaimaAPP NJOMBE
Mkuu wa mkoa wa Njombe Anthony Mtaka akihesabiwa mapema leo August 23 nyumbani kwake katika mtaa wa Lunyanyu ambapo mara baada ya kushiriki zoezi hilo akatumia fursa hiyo kuwahimiza wakazi wa mkoa wa Njombe kutosusia zoezi hilo muhimu kwa maendeleo ya taifa
Mtaka amesema kupitia takwimu zitakazopatikana mkoa wa Njombe utatumia kuweka mipango ya maendeleo na uchumi huku pia akisema kwakuwa mkoa huo unautajiri wa kutosha ambao unatokana na uzalishaji mkubwa wa mzazo ya chakula na biashara.
Lakini pia amesema tangu zoezi hilo lianze majira ya saa sita kamili usiku kwa kuandikisha watu katika maeneo maalumu zikiwemo hospitali,nyumba za kulala wageni na maeneo ya kulaza maroli hakuna hitirafu iliyojitokeza
0 Comments