Header Ads Widget

MBUNGE WA VITIMAALUM MARIAMU NYOKA ATOA VIFAA VYA MICHEZO KUHAMASISHA SENSA.



*********************

Na Amon Mtega,

Songea.

MBUNGE wa Vitimaalum kutoka Mkoa wa Ruvuma Mariamu Nyoka atoa vifaa vya michezo kwa timu za mpira wa miguu na mpira wa pete kwa lengo la kuhamasisha kushiriki Sensa na makazi August 23 mwaka huu.

Nyoka ametoa vifaa hivyo mipira na jezi mbele ya Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini Dkt Damas Ndumbaro ambaye pia ni Waziri wa Sheria na Katiba wakati wa kushiriki mbio za Sensa marathon ambazo zimekuwa rasmi kwa ajili ya kuhamasisha kushiriki zoezi la Sensa.

Mbunge Nyoka amesema kuwa ametoka vifaa hivyo kwa timu ambazo zimeshiriki zoezi la mbio za Sensa marathon ili kuunga mkono kazi zinazofanywa na Serikali juu ya zoezi hili la sensa.

Kwa upande wao wachezaji wa timu hizo mbili wamemshukuru Mbunge huyo kwa kupatiwa vifaa hivyo na kuwa watakuwa mstali wa mbele kuhamasisha wananchi washiriki zoezi la Sensa na makazi.

Naye muandaaji wa mbio za Sensa marathon ambazo zimekimbiwa klometa tano Dkt Damas Ndumbaro Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini amewashukuru wakazi wa Jimbo la Songea Mjini kwa kujitokeza kwenye zoezi hilo wakiwemo baadhi ya madiwani pamoja na Mbunge wa Vitimaalum Mariamu Nyoka.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI