Header Ads Widget

HAKUNA AGIZO LA KUCHANJA CHANJO YA UVIKO 19 KWA LAZIMA -WIZARA



WIZARA wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto imesema kuwa haijatoa agizo la wagonjwa wanaokwenda kutibiwa kwenye vituo vya Afya ama Hospitali za Serikali kulazimishwa chanjo ya UVIKO 19.


Mkurugenzi Msaidizi wa Elimu ya Afya kwa Imma Idara ya Kinga Wizara ya Afya Dr. Amalbega Kasangala aliyasema hayo Leo wakati akijibu maswali ya wanahabari mkoa wa Iringa waliotaka kujua kama ni lazima Kwa wagonjwa kuchanjwa Kwa lazima chanjo hiyo ya UVIKO 19 kabla ya kupata huduma ya matibabu aliyofuata .


Alisema kuwa   serikali haijalazimisha wananchi Kuchanja chanjo ya Uviko-19 na kuwa chanjo hiyo ni hiari ya mtu japo ni msaada mkubwa kwake.


Alisema serikali imelenga kuwakinga wananchi wake dhidi ya ugojwa huo.


"Tunatoa elimu kwa jamii ili itambue umuhimu wa kujikinga na ugonjwa huo    na zoezi hili ni muhimu na la hiari,hatulazimishi Ila ni muhimu watu wakachukua hatua," alisema Dr.Kasangala.


Pia amewataka wananchi kutoa taarifa za vituo vya Afya vinavyokataa kutoa Huduma kwa wagonjwa ambao bado hawajachanja kwa kuwa kufanya hivyo ni kosa kisheria.

"Sio maelekezo ya Serikali vituo vya Afya kutotoa huduma kwa mtu asiyechanja," alisema Dkt.Kasangala.  


Mganga Mkuu Mkoa wa wa Iringa alisema Hadi Sasa asilimia 50.2 tayari wamechanjwa Katika Mkoa huo.


"Hadi Sasa tumewafikia watu 303,747 wamechanjwa sawa na asilimia 50.2 ambapo wanatarajia kufikia asilimia 70 ifikapo mwezi Desemba.


Mkurugenzi mkazi wa Shirika la Marekani (USAID)  Katesomvongsiri alisema awali walitoa Dola milioni 25, na Sasa wameongeza Dola milioni 42 ili kuisaidia Tanzania kuendeleza mapambano dhidi ya Uviko-19.


Mkurugenzi huyo alisema fedha hizo zinazotolewa ni msaada na sio mkopo .

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI