Header Ads Widget

MASHIRIKA NA TAASISI (89) ZAPEWA RUZUKU YA BIL.4

 


Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma


MKURUGENZI  wa Shirika la Foundation For Civil ya Society  (FCS) Francis Kiwanga amesema Mashirika na Taasisi 89 zimepewa ruzuku ya bil.4 kati ya 1200 zilizoomba ili kutekeleza miradi ya kimaendeleo hapa chini.


Kazi kubwa zitakazofanyika na wadau hao ni kazi ya kusukuma ajenda ya utawala Bora nchini katika kuleta usawa wa kijinsia, Kufuatilia rasilimali katika sekta ya maji Elimu,Afya, kilimo na makundi maaluma.


Akizungumza leo Jijini Dodoma kwa AZAKI zilizochaguliwa kupata ruzuku alisema kuwa  FCS imejikita katika kuhakikisha miradi inayofadhiliwa inawasaidia wananchi katika kuboresha maisha maisha yao na kukuza  sekta ya asasi za kiraia.



Alisema kuwa taasisi zilizoomba zilikuwa zaidi ya 1200 kutoka Tanzania nzima lakini taasisi zilizofanikiwa 86 hivyo hizo fedha zimegawanywa kwenye mikoa yote na wadau wote ambao tunafanya kazi nao kwa mwaka huu.


Alisema kuwa wametoa ruzuku kiasi cha bil.4 kwa mwaka huu na wadau wote watafanya kazi kwa mwaka huu na mwakani,hivyo wameweza kupata wadau 86 wanaotoka katika  mikoa yote ya Tanzania bara na visiwani, ambao watakuwa wanafanya kazi kusukuma agenda ya utawala bora nchini.


“Lakini pia utawala bora katika maswala ya kuleta  usawa wa kijinsia , kufatilia rasilimali katika sekta ya maji ,elimu ,afya na kilimo na kufanya kazi na watu wa makundi maalum,kupiga vita juu ya ukatili wa kijinsia ,lakini pia kundi la vijana kuhakikisha rasilimali zinazotolewa na serikali na wadau wengine basi ziwe  zinawafikia watu hao”alisema.



Alisema kuwa eneo lingine wanalolifanyia kazi ni eneo la kutunza amani na utatuzi wa  migogoro Tanzania bara na Visiwani”Tunafahamu kwa sasa kumekuwa na  na ongezeko la migogoro kwenye rasilimali kama tunavyoona  sehemu zingine za wakulima na wafugaji wamekuwa na migogoro.


Hivyo basi kuna taasisi zaidi ya 10 ambazo zitakuwa zinafanya kazi katika utatuzi wa migogoro hapa nchini.


“Lakini pia serikali inamipango mingi sana na inapeleka rasilimali nyingi katika sekta ya kilimo hivyo sisi wajibu wetu ni hakikisha je rasilimali hizo zinawafikia walengwa,hivyo kupitia taasisi ambazo tumezichagua mwaka huu kuhakikisha eneo la kilimo kuna  ushirikishwaji mzuri wa wananchi lakini pia”.



Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Tanzania Women for Initiative Benadeta Choma alisema kuwa Ruzuku zinazotolewa na serikali na wafadhili zinawasaidia kujenga uelewa wa wananchi na hasa katika sekta ya afya ambapo wanaenda kuboresha afya ya wana jamii wa Wilaya ya Nkinga kwa kuona yale ambayo mpango mkakati wa wilaya ya mkinga ambao wapi wamefikia na wapi wamekwama na nini kifanyike kwahiyo mamlaka wanachukua hatua gani kuweza kuwasaidia watu wa mkinga.


Naye Meneja Program Utawala Bora Edna (FCS) Chilimo alisema kuwa wanamiradi katika maeneo mbalimbali kiwemo utawala bora maswala ya kijinsia,vijana na watu wenye ulemavu, ujenzi wa amani lakini pia wanamiradi mahususi kwaajili ya utawala bora katika sekta ya kilimo,afya ,elimu na maji.


“ Tunajengea uwezo Azaki ili ziweze kutekeleza miradi vizuri,kuweza kujiongoza,iwe imara na inayotambulika lakini pia tumechangia ukuaji wa sekta”alisema.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS