NA HADIJA OMARY MATUKIO DAIMAAPP LINDI
MKUU Wilaya ya Mtwara Dustan Kyobya amesema Maonesho ya nanenane yanatakiwa kuweka alama Chanya na kuwa na sura ya mabadiliko yanayoonekana kwa macho kwa wakulima ,wafugaji na wavuvi Mkoani Lindi wanaopata huduma na bidhaa katika maonesho hayo.
Kyobya ambae amemwakilisha mkuu wa mkoa wa Mkoa wa Mtwara katika ufunguzi wa maonesho ya sikukuu ya wakulima (Nanenane)kanda ya kusini yanayofanyika katika viwanja vya Ngongo manispaa ya Lindi mkoani Lindi ametoa Rai hiyo wakati alipotembelea katika banda la taasisi ya utafiti wa kilimo TARI kituo cha Naliendele.A
amesema kuwa licha ya taasisi hiyo kueneza teknolojia zinazotokana na tafiti Mazao katika maeneo mbalimbali hapa nchini lakini pia waendelee kuzitangaza bidhaa mbalimbali zinazotokana na zao la korosho hasa katika uongezaji wa mnyororo wa thamani wa zao hilo.
Alisema yapo mazao mengi ambayo yanatokana na korosho hivyo ni muhimu kuyatangaza ndani ya Mkoa, kupitia Maonyesho hayo , ngazi ya kanda na hata Nchi kwa ujumla ili kila mtu aweze kuona kwa Wingi
" Mazao yanayotokana na korosho yanatakiwa kutangazwa nimeona hapa mwenyekiti wa halmashauri ya Tandahimba amekunywa maziwa ya Korosho kwa niaba yetu lakini ukienda kuuza sehemu mbali mbali watu wengi watapata faida , je vikundi vya vijana akina mama na watu wa makundi maalumu kupitia mikopo ya asilimia 10 wakiwezeshwa na kupewa mashine si wanaweza kutengeneza wakauza " alisema kyobya.
Kwa upande wake Geradina Mzena Mratibu wa utafiti na ubunifu toka taasisi ya utafiti wa kilimo TARI kituo cha Naliendele amesema kupitia maonesho hayo TARI Naliendele imeandaa zoezi maalumu la kuhamasisha ulaji wa korosho litakalofanyika hapo kesho katika viwanja hivyo.
Kupitia maonyseho hayo amewataka wakulima na wadau mbali mbali kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kujionea bidhaa mbali mbali zinazotokana na zao la korosho pamoja na kushiriki kwa pamoja katika kula bidhaa hizo
Nae meneja wa benki ya NMB kanda ya kusini Janeth Shango amesema katika kuunga mkono kauli mbiu ya mwaka huu isemayo Agenda 10/30 Kilimo ni Biashara shirika kuhesabiwa Kwa mipango Bora ya Kilimo ,Mifugo na Uvuvi Bank hiyo imeandaa mikopo mbali mbali kwa wakulima , wafugaji na wavuvi ili kuweza kuwasaidia katika kuendeleza na kukuza Biashara zao
0 Comments