Header Ads Widget

DC LINDI - SHAHIBU NDEMANGA, WANANCHI POKEENI MAKARANI HAKUNA SWALI LENYE UKAKASI

NA HADIJA OMARY MATUKIOADAIMAAPP LINDI 

MKUU wa Wilaya ya Lindi amewataka wananchi kuwapokea makarani watakaofika kwenye maeneo yao na kuwapa ushirikiano wa kutosha kwa kutoa takwimu zilizo sahihi za wanakaya waliolala na kuamka katika nyumba zao 

Ndemanga ametoa rai hiyo mapema leo hii Agasti 23,2022 mara baada ya kufikiwa na karani wa Sensa Nyumbani kwake Mtaa wa Mtanda Manispaa ya Lindi Mkoani humo 

Ndemanga alitumia fursa hiyo kuwatoa wasiwasi wananchi wa Wilaya ya Lindi kuwa maswali yanayoulizwa na makarani wa Sensa ni mepesi  na kwamba  yanajibika kwa urahisi


" naomba niwatoe hofu wananchi wa Wilaya ya Lindi na Watanzania kwa ujumla kiufupi katika maswali yanayoulizwa na makarani hawa hakuna swali lenye ukakasi linaloweza kumfanya mtu ashindwe kujibu kwa urahisi"

Ndemanga alisema kuwa maswali yanayoulizwa na makarani wa Sensa ni mazuri na kwamba mtu yeyote alielala kwenye kaya husika anaweza kuyajibu

"Ukiyasikiliza Maswali haya unaona kabisa kuwa ni maswali ambayo yanataka kupata taarifa ambazo ni muhimu sana katika maendeleo ya Nchi yetu lakini na mke wangu tulikuwa tunaangaliana hapa kuona kuwa kumbe maswali haya ni muhimu hata kwa familia " alisema Ndemanga 


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI