Header Ads Widget

BILIONI 76 KUTUMIKA KUJENGA CHUO CHA UFUNDI LINDI

 


NA HADIJA OMARY, LINDI.


Serikali imetoa kiasi cha shilingi bilioni 76 kwa ajili ya ujenzi wa chuo cha ufundi Lindi (campus ya Arusha Techinical college) kinachotarajiwa kujengwa katika mtaa wa kikwetu manispaa ya Lindi Mkiani humo.


Chuo hiko kinachotajwa kuwa ni cha aina yake katika ukanda wa jangwa la Sahara  kitakapokamilika  kinatarajiwa kuchukuwa wanafunzi Zaidi ya mia 600.



Akizungumza na waandishi wa Habari  mratibu wa ujenzi wa chuo  hiko Dkt. Elick baada ya kutembelea Eneo litakalojengwa chuo hiko , alisema ujenzi huo unatarajiwa kuanza wakati wowote kuanzia sasa na kwamba kitakamilika mwezi Juni  mwaka 2023.


“ujenzi wa chuo cha ufundi lindi ni mwendelezo wa Mradi wa bwawa la mwalimu Nyerere agro power project ambapo serikali ilipata fedha hiyo kwa ajili ya CRS na kutenga kwa ajili ya vyuo vitatu ambavyo ni chuo cha Tehama Kigoma, Afya Domama na chuo hiki cha ufundi Lindi” alisema


“ chuo hiki pia  kitajengwa kwa usimamizi wa chuo cha ufundi Arusha na tunatarajia kuwa ni chuo bora katika ukanda huu wa kusini mwa jangwa la Sahara kutokana na kuwa na Mahabara  karakana na madarasa vyote vikiwa ni vya kisasa ambapo hata  program zitakazotolewa hapa ni zile fani ambazo zinauhitaji katika jamii ya Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla”alisema Dkt Mgaya.


Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Lindi Bi. Zaunab Telack alisema kuwa wapo tayari kwa kupokea mradi huo kwani utasaidia kunoa vijana wa mkoa huo kupata ujuzi utakaowasaidia kuingia kwenye soko la Ajira.


Naye msahiki meya wa manispaa ya Lindi Frenk Magali alisema kuwa kuwepo kwa chuo hiko mara tu kitakapokamilika ujenzi wake kitasaidia kuinua uchuma wa Manispaa ya Lindi na Mkoa kwa ujumla kutokana na ongezeko la watu.


MWISHO

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI