Na Matukio DaimaAPP
Watumishi wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania TARI kituo cha Naliendele wamelipongeza Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani kwakuwapa mafunzo ya udereva wa awali na usalama barabarani ambayo yalitolewa katika kituo hicho.
Akisoma hotuba ya wahitimu hao 55 Mtafiti wa kitengo cha Uhaurishaji Teknolojia na Mahusiano Gasper Mgimiloko alisema kuwa mafunzo hayo yamewapa upeo wa kufahamu aina za madereva.
Alisema kuwa kabla ya mafunzo hayo hakujua kama kuna dereva nyoka, kenge na kinyonga ambapo jeshi hilo limewaasa kuwa dereva kinyonga anayebadilika badilika ili kujali watumiaji wengine wa barabara.
“Tumepata bahati kupata mafunzo katika eneo letu la kazi hivyo tumepata muda mrefu wa kujifunza ambapo washiriki wote 55 walifika na kujifunza”
“Tulipata bahati pia ya kukijua chombo matumizi ya barabara udereva wa kujihami na dhana nzima ya ajali, bima na umuhimu na upatikanaji wa lesseni ikiwemo pia na maana na matumizi, ishara na alama za barabarani”
Mkurugenzi wa Tari kituo cha Naliendele Dr Furtunus Kapinga ambaye alikuwa ni mmoja kati ya wahitimu alisema kuwa mafunzo hayo yamewaongezea ufahamu juu ya matumizi sahihi ya barabara.
“Tumesoma mafunzo ya udereva wa awali na usalama barabarani ili kuweza kufahamu maboresho mbalimbali ya sheria za barabarani ambazo zinabadilika mara kwa mara mfano zipo alama za barabarani ambazo ziliwekwa zamani hivyo kupitia mafunzo hayo tulikumbushwa”
“Mafunzo yalikuwa ni muhimu kwa watumishi wangu kwakuwa waliyachukulia kwa uzito mkubwa hata mimi nimefurahia kuona wakisoma kwa moyo na kufahamu masuala ya usalama barabarani.
Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha usalama barabarani (trafiki) Wilaya ya Mtwara George Shimba alisema kuwa mafunzo hayo ni muhimu kwa kila mtu ni yanaweza kuwasaidia na kujiepusha na adhabu ama fine.
"Tumetoa mafunzo ya mafunzo ya udereva wa awali na usalama barabarani kwa Watumishi 55 wa TARI Naliendele elimu ambayo ni muhimu kwa kila kiumbe kinachotumia barabara.
“Kuna mtu aliyeelimika na asiye na anayesimamia utaratibu hii inaleta mkanganyiko ndio maana tunaona madhara yake ni makubwa kwakuhatarisha maisha ya wanatumia barabara hizo hivyo utolewaji wa elimu kama hii una faida kubwa kwa jamii”
“Elimu hii itutatumika barabarani na kuondoa msuguano ndani ya jamii na tuanaamini kuwa hawa waliopata elimu watatoa kwa wengine pia ili kutelekeza sheria bila shuruti” alisema George
0 Comments