Header Ads Widget

ADC YAWATAKA WANANCHI KUSHIRIKI ZOEZI LA SENSA

 


Na Fatma Ally Matukio Daima APP Dar es Salaam



Mwenyekiti wa Chama Cha ADC Taifa,Hamad Rashid amesema kuwa kila jambo la kitaifa litakalotokea katika nchi ya Tanzania chama chake kitashikiri kikamilifu kwani wao kufanya hivyo ni kujiandaa na kushika madaraka katika uchaguzi mkuu utakao fanyika mwaka 2025. 


Kauli hiyo ameitoa jijini Dar es Salaam leo wakati alipokua katika warsha fupi ya kutoa elimu kwa wanachama wao kuhusu kushiriki zoezi la sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika August 23 mwaka huu ambayo inalenga kujua idadi ya watu katika kupanga mipango ya maendeleo kwa Taifa na watu wake.


Amesema kuwa, ni muhimu sana wananchi kujitokeza kuhesabiwa katika sensa ya watu na makazi na kutoa taarifa sahihi ili Serikali itakapopanga mipango ya maendeleo iwe na takwimu sahihi, ambapo amesema katiba ya chama chao inaheshimu kiongozi aliyepo madarakani.



"Hivi karibuni tutasherehekea miaka 10 ya kuanzishwa chama chetu, ni chama makini sana na imara hakuna migogoro, katiba yetu inasema heshimuni aliyepo madarakani muda wenu ikifika mutachukua madaraka, hivyo lazima tushiriki sensa kwa ajili ya kujua watu tutakao waongoza"amesema Mwenyekiti Hamad.


Aidha, amewataka viongozi wa chama hicho kuendelea kushirikiana na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu, huku akiwataka wananchi kuacha itikadi za kimila na kidini na kujitokeza tarehe 23 kwa ajili ya kuhesabiwa.


Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Chama hicho Doyo Hassan Doyo amewataka mawakala wa sensa watakapofika sehemu za vijijini kuwa wakarimu na wananchi wa huko Ili kuepuka kutopewa taarifa ambazo sio sahihi kwa watu kuhofia wakitoa taarifa zao wataweza kulipishwa ushuru wa nyumba zao.




"Sisi chama Cha ADC tumekua tukitoa elimu kwa wananchi kuhusu kushiriki zoezi la sensa kwa ajili ya mipango ya maendeleo muda mrefu lakini taarifa zilizopo huko ni kwamba wakitoa taarifa zao wataweza kulipishwa ushuru katika nyumba, hivyo nitoe rai kwa wasimamizi wa sensa lazima wapange watu ambao ni watu wa eneo husika Ili waweze kupata taarifa sahihi"amesema Doyo.


Aidha amewataka wazazi kuwafichua watoto wao wenye ulemavu Ili waweze kuhesabiwa kwani haki yao ya msingi, hivyo wasiwafungie ndani watashindwa kuingizwa katika mipango ya maendeleo katika eneo husika kwani Ili maendeleo yaweze kufanyika ni lazima kupatikana takwimu sahihi.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI