Na Fatma Ally Matukio Daima APP Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi Vijana Ajira na watu wenye ulemavu) Prof Joyce Ndalichako ameyataka mashirika yote ya umma na binafsi pamoja pamoja na wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuwasilisha michango ya wanachama wao kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii Ili mifuko hiyo iweze kuwalipwa kwa wakati wanachama wake.
Agizo hilo amelitoa jijini Dar es Salaam leo wakati alipokutana wazee wastaafu wa mifuko ya PSSSF na NSSF katika mkutano maalum wa kupokea maoni na kutatua changamoto za ulipwaji wa mafao ambapo amesema kumekua na changamoto mbalimbali kwa wastaafu hasa katika mafao wanayopokea hayaendani na mishahara waliokuwa wakipokea.
Amesema kuwa, wastaafu wengi waliofika katika Mkutano huo changamoto zao zinatatulika na wengine malalamiko yao ni mapunjo ya mafao wanayopokea ikilinganishwa na mishahara waliokuwa wakipokea, hali ambayo imechangiwa na kikokotoo walichofanyiwa hakiendani na mishahara na mshahara halisi waliokuwa wakipokea.
"Wamefanyiwa kikokotoo kwa mshahara ambao sio halisi, nilichokiona hapa wamepigiwa hesabu kwa mishahara ambayo sio yao na kusababisha mafao yao kuwa kidogo kuliko inavyotakiwa na pensheni yake ya mwezi pia inakua ndogo"amesema Waziri Prof Ndalichako.
Aidha, amewataka watendaji wa mifuko hiyo ya hifadhi ya jamii kuwaondolea ukuta wananchi wanapokwenda kutaka huduma ikiwemo ikiwemo kuonana na watendaji wakuu kwa ajili ya kuelezea malalamiko yao juu mafao yao kuwa madogo.
"Kuanzia leo naomba kuta zote zivunjwe muachie watu wafike kwa wenye maamuzi na changamoto zao, kama mimi Waziri nimeweza kuondoka ofisi kwangu na nikawafata huku wastaafu kwa nini nyie watendaji ngumu kumruhusu mtu kuonana na watendaji wakuu"amesema Waziri Prof Ndalichako.
Aidha, amesema changamoto nyengine ni kuhusu watu waliohama kutoka mfuko wa NSSF na kwenda PSSSF, ameeleza kuwa ikiwa mtu amechangia kwenye mfuko chini ya miezi 12 basi anatakiwa abaki kwenye mfuko wake wa zamani na ikiwa amezidi miezi 12 basi abakie kwenye mfuko wake mpya.
Kwa upande wake,Chiku Said ambae ni miongoni mwa wastaafu waliofika katika kikao hicho cha kupeleka malalamiko kuhusu mafao amesema amefanya kazi na Wizara ya Afya tangu 1973 na kustaafu mwaka 2014 hadi kufikia Leo Julai 22, mwaka 2022 hajapata mafao yake licha ya kufuatilia mara kadhaa.
"Huu ni mwaka wa tisa tangu nilipostaafi kufanya kazi lakini nazungushwa mara naambiwa niende nikafatilie Dodoma naenda, mara nirudi Dar es Salaam sijapata muelekeo wowote wa mafao yangu, leo nimekuja kuonana na Waziri naamini nitaweza kupata haki yangu maana nimezungushwa sana" amesema Chiku.
0 Comments