Na Gabriel Kilamlya ,MATUKIO DAIMAAPP NJOMBE
Wakati zoezi la kusaka vipaji kwa vijana wenye uwezo wa kucheza mpira wa miguu mkoani Njombe likitarajiwa kuhitimishwa siku ya Jumapili pale Mtwango vijana wenye uwezo huo wametakiwa kujitokeza kwa wingi ili waweze kuitumia fursa hiyo kuonyesha vipaji vyao.
Akizungumza na waandishi wa habari mkurugenzi wa Idara ya mawasiliano Njombe fc Sophia Issa amesema wakati zoezi hilo likiendelea mpaka sasa jumla ya vijana 48 wamepatikana na wanajindaa kuripoti katika kambi za Njombe fc tarehe 29 mwezi huu.
Katika hatua nyingine Sophia Issa ameviomba vyama vya soka vya wilaya zote za mkoa wa Njombe kuona namna ya kuwatumia katika mashindano mbalimbali wachezaji watakao kuwa wamesalia katika zoezi hilo ili waendelee kuonyesha vipaji vyao.
Kama wewe ni kijana mwenye uwezo wa kucheza mpira wa miguu hii ni fursa kwako ichangamkie ili ndoto yako itimie.
0 Comments