Header Ads Widget

VIJANA WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA KUJITUMA

 



Na Gift Mongi Moshi


Katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro Willy Machumu amewataka vijana kufanya kazi  kwa kujituma sambamba na kuongeza ubunifu  kwani hali halisi ya maisha siyo rahisi kama wanavyofikiria.


Machumu alitoa rai hiyo katika kongamano la wafanyabiashara na wajasiriamali lililoandaliwa na diwani wa Uru Kusini  Wilhad Kitally,ikiwa ni maadhimisho ya sikukuu ya wafanyabiashara.


Alisema wafanyabaishara wengi waliofanikiwa imetokana na jitihada binafsi katika kujituma lakini pia kuwa na malengo ambayo yanatekelezeka hivyo kuwa nyenzo muhimu katika kuyafikia mafanikio.


"Naomba kuwaasa wazazi kuwapa elimu watoto wenu sambamba na malezi yaliyo bora ila kama mnaona elimu Ni ghali jaribuni ujinga"alisema



Kwa upande wake mbunge wa Moshi Vijijini  Prof Patrick Ndakidemi alisisitiza vikundi vya vijana, wanawake na walemavu kuchangamkia fursa ya mikopo isiyokuwa na riba kutoka halmashauri.


Alisema kutokana na serikali kuona makundi hayo kwa kipindi kirefu yanakosa mitaji katika kujiajiri na kuendesha shughuli zao ndipo ulipoanzishwa mkakati huo wa kutoa mikopo isiyo na riba hivyo kila mwenye sifa anaweza kunufaika.


"Ipo haja Sasa kwa makundi haya Kama vijana wanawake na wenzetu wenye ulemavu kuona umuhimu wa kuchangamkia fursa hizi za mikopo ili kuweza kujikwamua kiuchumi"alisema


Naye diwani Uru Kusini, Wilhad A. Kitaly aliwashuku wananchi, wajasiriamali na wafanyabiashara wote waliohudhuria kongamano kwa kushiriki kupata maarifa na elimu kuhusu fursa mbalimbali za biashara.


Pia  aliwahasa vijana kutochagua kazi za kufanya na kujitahidi kubadili changamoto kuwa fursa ili kuweza kujipambanua zaidi katika kupambana na uhaba wa ajira.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI