Header Ads Widget

WANAFUNZI WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA KUSOMEA KISWAHILI

 



 Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma



IKIWA ni mara ya kwanza kwa Kiswahili kusherehekewa duniani tangu kutengewa siku yake maalum na Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) mnamo Novemba 23, 2021 wito umetolewa kwa wanafunzi kuchangamkia fursa ya kusomea lugha ya kiswahili .


Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo Haji Janabi  

wakati wa  alipokuwa akiwapa vyeti wahitimu wanaosoma Lugha ya kiswahili kwa ajili ya kuwafundisha wageni huku akisisitiza kuwa Lugha ya kiswahili sasa ni Lugha ya dunia kwani kila nchi mbalimbali zimeanza kufundisha huko duniani.


Alisema kila tarehe 7 ya mwezi Julay ni siku ya kiswahili duniani na kwa sasa kiswahili ni bidhaa hivyo wahitimu wote waliosoma somo hilo wataingizwa katika Mfumo utakao watambua Kama wahitimu mahili wa Lugha ya kiswahili kwa kuingizwa kwenye Kanzi data. 



"Niwaombe msiishie hapa jifunzeni na Lugha nyingine mbalimbali ili muendane na soko la dunia kumbukeni washindani wetu wapo kutoka nchi jirani Kenya Uganda bila kuwasahau wachina na soko ni moja tu juhudi zenu za kujifunza na kufanya kwa umahili ndicho kitu kitakachowafanya mfanikiwe,"alisema Janabi


Na kuongeza Kusema"Bado mna safari ndefu kwani kujua kiswahili pekee haitoshi na sio kupata ajira hiyo ni wakati Sasa wa kuchangamkia na kujifunza Lugha zingine  mbalimbali japo najua hamuwezi kusoma Lugha zote," alisema Janabi 


Awali akiongea kabla ya ugawaji wa vyeti kwa wahitimu hao wanaosomea lugha ya kiswahili kwa ajili ya kuwafundisha wageni Mkufunzi wa mafunzo kutoka baraza la kiswahili Tanzania Bakita Wema Msingwa alisema mafunzo hayo yalianza kufundishia 2018 baada ya agizo la aliyekuwa Waziri wa utamaduni sanaa na Michezo Dkt Herison Mwakyembe na baada ya wataalamu kujiajili katika kanzidata ndipo walipoanza kufundisha pale Baraza la kisawahili na baadae wakawa wanawafuata wahitimu wa vyuo vikuu  katika vyuo vyao.


Alibainisha kwa  awamu ya kwanza waliwapata Wanafunzi 28 ambapo waliendelea kutafuta Wanafunzi wengine katika vyuo ambapo mpaka Sasa wameshafundisha na kusajili wanafunzi wapatao 1417 katika kanzidata.


Aidha alieleza katika chuo kikuu Cha Dodoma UDOM wamewasajili Wanafunzi 210  na lengo lao ni kuwafundisha Wanafunzi wote waliojisajili katika kanzidata.


Naye Mwakilishi wa mkuuu wa Idara ya kiswahili Udom Dkt Boniface Alphonce  alisema Lugha ya kiswahili ni biashara na ni mtaji na endapo kiswahili kikitumika vizuri manufaa yapo tena makubwa.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI