Tume ya vyuo vikuu Tanzania-TCU- imefungua dirisha la udahili kwa wanafunzi wa elimu ya juu kuanzia tarehe nane Hadi tarehe 15 mwezi huu kwa ajili ya mwaka.wa masomo 2022/2023.
Katibu mkuu mtendaji wa tume hiyo Profesa Charles Kihampa alisema tume inawahimiza waombaji kupata Taarifa sahihi kupitia tovuti ya TCU na vyuo vyuo vilivyotuhusiwa kidahili wanafunzi na kusikiliza taarifa mbalimbali kupitia vyombo vya habari.
"Udahili huo utakuwa katika makundi matatu ambayo ni wanafunzi wenye sifa za stahiki kidato Cha sita,stashaha au sifa zinazolinganifu na wenye sifa stahiki za cheti Cha awali kutoka chuo kikuu huria."Alisema profesa Kihampa.
Pia aliongea kuwa ili kutambua sifa hizo za makundi wanafunzi wanatakiwa kusoma vigezo katika vitabu vya mwongozo vya TCU vinavyopatikana katika mtandao wa tovuti ya TCU- ambayo ni www.tcu.go.tz.
Pia ametoa wito kwa waombaji wa udahili na wananchi kujitokeza katika maoneshonya 17 ya elimu ya juu Sayansi na Teknolojia yatakayofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijin Dar es Salaam kuanzia tarehe 18 julai Hadi tarehe 23 Julia mwaka huu ili kupata Taarifa mbalimbali kuhusiana an vyuo.
Hatahivyo aliwaondoa hofu wazazi na vijana waliojiunga na jeshi la kujenga Taifa.JKT - kwa mujibu wa Sheria kuwahakikisha vijana hao watapata msaada wa kudahiliwa kutokana na utaratibu unaofanywa na Jeshi Hilo.
Pia alisema katika vyuo vya elimu ya juu hapa nchini hakuna mawakala hivyo wananchi hawana budi kuwa makini katika udahili wa masomo kwa vyuo mbalimbali.
0 Comments