Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limebainisha kuwa, imegundua kiasi kikubwa cha gesi asilia futi za ujazo trilioni 57.54 ambapo mchakato wake ukikamilika wataweza kuimalisha soko la ndani na kuuza nje.
Amebainisha hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dk. James Mataragio katika Maonyesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba ambayo yanaendelea kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam
Ambapo amesema kiasi kikubwa cha gesi hiyo, kimegundulika baharini.
“Kiasi kikubwa cha gesi kipo baharini, tunatarajia kukivuna, kwasasa tunaendelea na mtambo wa LNG ambao utachakata gesi hiyo,” alisema Dk. Mataragio.
Dk. Mataragio ameongeza kuwa, mchakato wa gesi hiyo itakapokuwa umekamilika itasafirishwa kwenda kwenye masoko ya nje na kwamba kiasi kitakachobaki kitatumika kwa ajili ya soko la ndani.
Aidha, amebainisha kuwa, wanaendelea kujenga vituo vingine zaidi ilikusogeza huduma kwa wananchi, mchakato ambao utakamilika mwakani.
“Tutakuwa na vituo zaidi, Mteja atakuwa anaenda kwenye vituo vyetu ili kuweza kuweka gesi anayoihitaji." Alisema Dk. Mataragio.
Aidha, gesi asilia imekuwa na matumizi makubwa ikiwemo kuzalisha umeme ikichangia asilimia 62 kwenye gridi ya taifa.
0 Comments