Header Ads Widget

SERIKALI YA KOREA YAIPATIA TANZANIA MKOPO WENYE MASHARTI NAFUU

 


NA HAMIDA RAMADHAN ,MATUKIO DAIMAAPP,DODOMA

SERIKALI imekopa mkopo wa Masharti nafuu kutoka ufadhili wa serikali ya Korea lengo likiwa ni kutekekeza mradi wa uboreshaji wa huduma ya maji taka unalenga kuhudumia kata 11 na kuboresha mtandao uliopo katika kata 14.


Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji DUWASA Mhandisi Aron Joseph alipokuwa akieleza utekekezaji  wa shughuli za mamlaka ya maji na usafi wa Mazingira Dodoma DUWASA na muelekeo wa utekekezaji wa mwaka wa fedha 2022/2023 ambapo Alisema Mradi huo utaweza kutibu majitaka lita milioni 20 kwa siku.


Mhandisi Aron Alisema Mradi huu utahusisha ujenzi wa mabwawa 16 eneo la Nzuguni Utaongeza mtandao wa majitaka usiopungua kilomita 250 na  mradi utaunganisha wateja wasiopungua 6,000 pia Utaongeza huduma ya usafi wa Mazingira kutoka asilimia 20 hadi 45.Mradi una gharama ya Tsh. 161bn. 


"Mradi upo katika hatua za mwisho za kumpata Mkandarasi Mshauri na Mradi wa Majitaka na uboreshaji huduma ya Majisafi kwenye Mji wa Serikali", 


Alisema Serikali kupitia Wizara ya Maji kwa kushirikiana na DUWASA ipo katika hatua za mwisho kusaini mkataba na Mhandisi Mshauri. 



Mradi huu unatarajiwa kugharimu takribani shilingi za Tanzania Bil. 94, ambazo zimeshatengwa na Serikali Kuu.



UKUMBUSHO KWA WANANCHI



Mhandisi Aron aliwataka wananchi kutunza miundombinu ya majisafi na majitaka Lakini pia kutunza vyanzo vya maji kwa kuboresha mazingira hasa upandaji na utunzaji wa miti.


Pia aliwaomba wananchi kuwa na matumizi sahihi ya maji na kuhifadhi maji,Matumizi sahihi ya mtandao wa majitaka.


"Pia naomba niwakumbushe wateja wote wa DUWASA kulipa Ankara zao kwa wakati ili kuzuia usumbufu wa kukatiwa maji," Alisema Mhandisi


Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI