Na Hamida Ramadhan Matukio Daima App Dodoma
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Antony Mtaka amewataka wafanyabiashara na wajasiriamali wa Mkoa wa Dodoma kuendelea kuchangamkia fursa zilizopo ndani ya Mkoa huo badala ya kuwa watazamaji.
Mtaka ameyasema jijini Dodoma wakati akizungumza katika kongamano la wajasiriamali na wafanyabiashara la ‘’Dodoma Business Forum’’ ambapo amesemakuwa Mkoa wa Dodoma una fursa nyingi ambazo wajasiriamali na wafanyabiashara wa bado hawajazitumia.
‘’Niwaombe wafanyabiashara na wajasiriamali mlioko Dodoma msiwe watazamaji,watu wanatoka katika mikoa mbalimbali wanakuja kuchukua fursa nyie mpo tu,changamkieni fursa zilizopo ,kwa mfano Dodoma inapokea wageni wengi kila siku na pia kuna mikutano mikubwa inayofanyika mara kwa mara kama wajasiriamali mnaweza kutumia fursa hiyo kuuza bidhaa zenu na mkapata fedha’’Alisema Mtaka.
Naye Mbunge wa jimbo la Dodoma Mjini na Naibu Waziri wa Kilimo Antony Mavunde amewapongeza wajasiriamali wa Dodoma kwa kuamka na kuanza kuandaa makongamano mbalimbali ya kupeana elimu kuhusu biashara na masoko.
‘’Kwakweli niwapongeze sana wananchi wa Dodoma sasa mmeanza kuamka , najua hapa mnapeana Elimu na ujuzi mbalimbali wa kufanya biashara na kupata wateja na niwaombe mtumie majukwaa haya vizuri ili yawe na matokeo kwenu’’ Mavunde
Nae muandaaji wa kongamano hilo Elizabeth Ngede amesema nia ya kuandaa jukwaa hilo ni kuwakutanisha wafanyabiashara na wajasiriamali mbalimbali wa Mkoa wa Dodoma ili kuwapa elimu ya biashara na kutokufanya biashara kwa mazoea kwani hilo ndiolimekuwa tatizo kubwa wa walio wengi.
Aidha akieleza sababu za wafanyabiashara wengi kushindwa kurejesha mikopo wanayokopeshwa na Taasisi mbalimbali ,Ngede amesema kuwa tatizola wafanya biashara wengi wanakopa ili kuanzisha biashara badala ya kukopa ili kuendeleza biashara
‘’Ni kweli kumekuwa na wafanyabiashara wengi wanaoshindwa kurejesha mikopo wanayokopeshwa na Serikali au Taasisi binafsi lakini mimi niwashauri wasikope ili kuanzisha biashara hii ni hatari bali watu wakope ili kuendeleza biashara hii ni afadhali kwao kwa sababu mtu anakuwa tayari na uelewa wa kile anachokifanya’’Aliongeza Ngede






0 Comments