Mwenyekiti wa kamati ya maonesho ya nanenane kanda ya ziwa magharibi Mkuu wa Mkoa Mhandisi Robert Gabriel ameyataka mashirika, kampuni, Asasi, Taasisi na wadau mbalimbali kujitokeza katika kushiriki maonesho hayo.
Maonesho hayo yatakayofanyika kuanzia Agosti 1-8 katika viwanja vya Nyamhongolo Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza yakiwa na kauli mbiu isemayo ajenda kumi thelathini kilimo ni Biashara.
Mhandisi Gabriel ametaja baadhi ya Mikoa itakayoshiriki katika maonesho hayo ya Nanenane ni pamoja na Kagera, Mwanza pamoja na Geita na kuwataka wadau kushiriki ili kuonesha na kutangaza bidhaa na huduma mbalimbali walizonazo.










0 Comments