Header Ads Widget

UGONJWA USIOJULIKANA MKOA WA LINDI NI HOMA YA MGUNDA

NA HADIJA OMARY ,MATUKIO DAIMAAPP,

LINDI

Waziri wa Afya Mheshimiwa Ummy Mwalimu amesema kuwa upimaji wa sampuli za wagonjwa   Usiojulikana  waliokuwa wakiugua wananchi katika Wilaya ya Ruangwa  Mkoa wa Lindi umethibitisha mlipuko huu kuwa wa ugonjwa wa Leptospirosis, Field Fever ( homa ya Mgunda)

Waziri Ummy ameyasema hayo leo mara baada ya kufanya zihara Wilayani Ruangwa mkoani Lindi na kuzungumza na waandishi wa habari na timu ya wataalamu iliyopo Wilayani humo kwa ajili ya kucanya uchunguzi juu ya ugonjwa huo. 

Ugonjwa huo wa Mgunda ni miongoni mwa magonjwa yanayoambukizwa kutoka kwa wanyama  kwenda kwa binaadamu na unasababishwa na Bakteria aina ya leptospira interrogans .

Aidha alisema kuwa ugonjwa huo umekuwepo katika maeneo ya kitropic ambayo ni yenye hali ya joto katika mabara ya Amerika ya kasikazini, amerika ya kusini , Afrika, Asia na Australia

 Alisema wanyama aina za panya ,  kindi , mbweha , kulungu , swala na wanyama poli wengine wameripotiwa kupata maambukizi ya vimelea hivyo na kuwa chanzo cha maambukizi kwa binaadamu


Hata hivyo Waziri Ummy alieleza kuwa ugonjwa huo kwa Nchini Tanzania sio ugonjwa mpya kwamba ulishawahi kutokea  mwaka 2014 katika halmashauri ya Buhingwa Mkoani kigoma

Aidha aliongeza kuwa Ugonjwa huo wa Mgunda huambukizwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa binaadamu kupitia uchafuzi wa mazingira ikiwemo vyanzo vya maji kutoka katika mkojo wa wanyama , wenye maambukizi ambapo maambukizi hayo uenda kwa binadamu kupitia njia ya kugusa mkojo au maji mengone ya mwili kutoka kwa mnyama mwenye maambukizi , kugusa maji, udongo au chakula kilichochafuliwa na mkojo wa wanyama wenye maambukizi

Njia nyingine ni kunywa maji yaliyochafuliwa na vimelea vya bakteria wa ugonjwa huo  pia ugonjwa huo unaweza pia kuingia mwilini kupitia ngozi au utando wa mucous ( macho , pua au mdomo) na kupitia ngozi yenye mikwaruzo ambapo hata hivyo uwezekano wa ugonjwa huo kuambukizwa kutoka kwa binaadamu kwenda kwa binadamu mwingine ni nadra sana  

“Wizara inaendelea kuchukua hatua za kukabiliana na ugonjwa huu na kuendelea kutoa taarifa kwa umma kuhusu mwenendo wa ugonjwa huu. Hivyo Serikali inawaasa Wananchi kutokuwa na hofu kwani ugonjwa huu unaendelea kudhibitiwa” amesema Waziri Ummy Mwalimu

Awali Mganga Mkuu wa Mkoa wa Lindi Kheri Kyaga wakati akitoa taarifa juu ya walichogundua wakati wa ufuatiliaji aliesema jumla ya  watu 20 walibainika  kuugua ugonjwa huo ambapo  asilimia 75 ya waliougua ni wanaume huku asilimia 15 ikiwa ni  Wanamake  na watatu kufaliki Dunia

 Kyaga aliongeza kuwa  katika ufuatiliaji wao kwenye eneo ambalo umeripotiwa ugonjwa huo  zipo taarifa za binadamu kula wanyama waliokufa na pia kwenye eneo hilo kuna vyanzo viwili tu vya maji ambavyo vinatumika na binadamu na wanyama


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI