Na Brighton Masalu, Dodoma
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Samia Suluhu Hassan, amefanya mabadiliko makubwa ndani ya Jeshi la Polisi.
Katika manadiliko hayo, Rais Samia amempandisha cheo aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai ( Director of Criminal Investigation - DCI), Kamishna wa Polisi (CP), Camillus Mongoso Wambura, kuwa Inspekta Jenerali na Mkuu mpya wa Jeshi la Polisi, akichukua nafasi ya IGP, Simon Nyakoro Sirro, aliyeteuliwa Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe.
Aidha, Rais Samia amempandisha cheo Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Ramadhani Kingai, kuwa Kamishna wa Polisi na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, akichukua nafasi ya Kamishna Camillus Wambura, aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi.
Katika mabadiliko ya hivi karibuni, ACP Kingai aliteuliwa kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, akitokea Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, katika mabadiliko madogo ya makamanda wa Polisi nchini.
Pia, Rais Samia amemteua aliyekuwa Mkuu wa Operesheni wa Jeshi la Polisi, Kamishna Liberatus Materu Sabasi, kuwa Mkurugenzi wa Fedha na Logistics.
0 Comments